2012-12-28 15:31:21

Vijana wanajumuiya wa Taize toka Ulaya wakusanyika Rome


Vijana wanajumuiya wa Taize wapatao arobaini elfu wamekusanyika jijini Roma kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wao wa 35 , ulioanza 28 Desemba hadi 2 January 2013. Jumamosi vijana hao watakutana na Baba Mtakatifu Benedikto XV1.
Hija hii ya vijana, kama ilivyoitwa , Hija ya UamInifu , ni tukio la mikutano ya sala na ibada, zitakazo fanyika katika makanisa mengi makuu ya hapa Rome na pia kutakuwa na warsha na majadiliano yatakayo fanyika katika vikundi vidogo vidogo kulingana na lugha wanazozungumza kwa ajili ya kuitazama Imani yao kwa kina.
Vijana wa Taize ni mfumo wa jumuiya ya kiekumene , inayowanuganisha vijana wa imani mbalimbali, na mikutano yake ya mwaka, inaendelea kuwa kivutio kwa watu vijana, kutaka kuona kile kinachowaunganisha, licha ya kuwa waumini wa makanisa mbalimbali kama Katoliki, Makanisa ya Mashariki au makanisa ya Kiprotestant.
Ni watu vijana wanaomtafuta Mungu na wanatamtafuta katika umoja wao, katika msisitizo wa maisha kimonesteri, kama mahali muhimu maalum kwa ajili ya kushirikishana uzoefu katika mazingira ya kimataifa.
Mkutano wa Taize ni kipindi cha sala, majadiliano na utendaji wa pamoja, kuona jinsi inavyowezekana kuishi kwa amaani na utulivu bila kujali mipaka ya kiinchi, kikabila au kimbali.
Jumuiya inatoa mwaliko kwa vijana wote kuacha kuwa na uvivu katika kuyaishi maisha ya kushirikishana , badala yake wajiunge katika utedaji thabiti wa Taize , ishara ya uekumene.
Kati ya wanaohudhuria mKutano huu wa Rome, ni Kijana Mkongwe katika jumuiya ya Taize, Bruda Paolo , mzaliwa wa Uingereza ambaye amekuwa wanachama wa Taize kwa zaidi ya miongo mitatu.








All the contents on this site are copyrighted ©.