Papa atafakari maisha ya mfia dini wa kwanza Mtakatifu Stefano
Maadhimisho ya Siku Kuu ya Mtakatifu Stephano ni wito katika kubadili maisha yetu.
Jumatano hii, ambamo Mama Kanisa ameadhimisha Siku Kuu ya Makatifu Stefano, Baba
Mtakatifu Benedikto XV1, hakutoa Katekesi yake kwa mahujaji na wageni,akiwa ndani
ya ukumbi kama ilivyo kawaida yake kwa siku ya Jumatano. Lakini alijitokeza dirishani
kwa nia ya kusali sala ya Malaika wa Bwana, pamoja na wote waliokuwa wamekusanyika
katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtaktifu Petro. Na aliutumia muda huo mfupi, kwa
mara ingine kutoa salaam zake za matashi mema kwa siku Kuu ya Noel, hutuba fupi ambayo
aliiangalisha katika siku kuu ya Kiliturujia ya Mtakaifu Stefano, Katika hotuba
hiyo alisema, katika kuiadhimisha Siku Kuu ya Mtakatifu Stefano, tunaalikwa kuitazama
sana sura ya Mwana wa Mungu , ambamo kilele cha furaha ya Noel, kinatuongoza kulitafakari
fumbo la Umwilisho wake. Na kwa ubatizo na Kipaimara , na kwa thamani ya zawadi
ya imani inayolishwa na Sakramenti za Kansia , na hasa Ekaristi Takatifu , tunajawa
na imani kwa Yesu Kristu kwamba, tumefungamana nae na anaendelea kutaka kubaki ndani
mwetu, ili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, tuiendeleze kazi yake ya kuufikisha ujumbe
wa wokovu kwa watu wote, huku akituongoza katika ukamilifu. Hotuba ya Papa inaendelea
kueleza, kuvutiwa na Kristo, kama alivyokuwa Mtakatifu Stefano, ina maana ya kuyafunua
maisha katika mwanga wa wito wake, ni kufanya mabadiliko na kuongoza katika njia ya
wema na ubinadamu kama upendo wa Mungu unavyotufundisha.