Mkesha wa Noel, sita wafariki kwa shambulio Kanisani- Nigeria
Kipeo cha mashambulizi dhidi ya Wakristu Nigeria bado ni kitisho. Jumanne wakati wa
adhimisho la Siku Kuu ya Noel, maghaidi wenye silaha walishambulia Kanisa katika Jimbo
la Yobe, Kaskazini mwa Nigeria. Shambulio lililosababisha watu sita kufariki duniani
kati yao akiwemo Padre. Na pia nyumba zisizopungua 20 kuchomwa moto na watu wanaodhaniwa
kuwa mashabiki wa Kiilslamu, wa kikundi cha Boko Haram. Kikundi hicho kikiwa
na silaha kali, kilishambulia kanisa wakati Wakristu wakiwa katika Ibada ya Mkesha
wa Noel katika eneo la vijijini la Peri, nje kidogo ya Mji wa Biashara wa Potiskum.
Washambuliaji hao. Hili ni shambulio jingine la umwagaji wa damu ya watu wasiokuwa
na hatia, Akito maelezo juu ya mashambulio hayo , Rais wa Chombo kinacho waunganisha
Wakristu Nigeria (CAN), Mchungaji Ayo Oritsejafor, kw amasikitiko makubwa ameyaita
mashambulio hayo, kuwa ni kitendo cha kinyama dhdi ya watu wanaotumia haki yao ya
kuabudu kwa amani.Na kwamba, huo ni uchoikozi na M maudhi yasiyo kifani, na unyama
mkubwa. Na ni kuwa kinyume kabisa na imani ya dini yoyote ile ianyosadiki kwa Mungu.
Amewasihi wananchi wema wa Nigeria, kutoanzisha mashabulizi dhidi ya uchokozi
huo, na badala yake , waendelee kukemea vikali uhalifu huu na kuchukua hatua madhubuti
si kwa njia ya jicho kwa jicho lakini , kupitia njia ya majadiliano na elimu ya umma
kama hatua za kukomesha unyama huo. Na wasiyakimbia maeneo yao ya kuzaliwi, bali wabaki
katika makazi yao, kwani ipo siku amani na utulivu vitarejea. Baba Mtakatifu Benedikto
XV1, Jumanne wakati akitoa ujumbe wake kwa jiji na dunia, alilikumbuka taifa la Nigeria
na kukemea mashabulio ya kighaidi yanayoendelea kumwaga damu za watu wasiokuwa na
hatia katika taifa hilo. Papa ameomba kuzaliwa kwa Kristu na kuwezeshe kurudisha
amani na mapatano nchini Nigeria, ambako matendo ya ugaidi mkatili unaendelea kuvuna
waathirika, hasa miongoni mwa Wakristo. Na pia Mkombozi wa dunia na awe msaada
na faraja kwa wakimbizi kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na
kwa ajili ya amani nchini Kenya, ambako pia kumekuwa na mashambulizi ya kikatili kwa
raia wema, na maeneo ya kuabudu.