Hakuna sababu ya kupoteza tumaini - kwa kuwa ukweli umezaliwa - Papa
Baba Mtakatifu Benedikto XV1, katika ujumbe wake kwa jiji la Roma na dunia kwa ujumla"Orbi
et Urbi, amehimiza watu kujenga tumaini la amani hata katika hali ngumu na hatarishi,
kwa kutegemea ukweli uliozaliwa Bethlehem pangoni. Veritas de terra orta est!" Papa
amesema, Wapendwa ndugu zangu wake kwa waume, wakazi wa jiji la Roma na duniani kote,
Krismasi Njema kwenu nyote na familia zenu. “Katika Mwaka huu wa Imani, ninapenda
kutoa salaam zangu za mataishi mema ya Noel, kwa maneno kutoka ya Zaburi: "Ukweli
unachipuka katika nchi". Na kufafanua, hasa , katika ukweli wake , Mzaburi, alilenga
katika siku zijazo:ambamo "Wema na ukweli vitakutana; / haki na amani vitakumbatiana
/ Ukweli atachupuka nje ya nchi, / na haki itaangalia chini kutoka mbinguni. / Bwana
mwenyewe atawapa mafao yake; / nchi yetu itaongeza matunda yake. / Haki itakwenda
mbele yake / na wokovu, sambamba katika njia ya hatua zake "(Zab 85:11-14).
Leo
maneno haya ya kinabii yametimia . Kwa Yesu, kuzaliwa Bethlehem na Bikira Maria,
wema na ukweli hakika vimekutana, haki na amani vimekumbatiana; ukweli umejichomoza
kutoka katika nchi na haki imetazama chini kutoka mbinguni. Papa pia amerejea
maelezo ya Mtakatifu Augostine, anaye toa jibu fupi la kustaajabia, "Ukweli ni kitu
gani? Ni Mwana wa Mungu. Na je, ni nchi?Ni mwili. Kwa kujiuliza Jinsi Kristu alivyozaliwa,
utaona ukweli kwamba, ukweli umejitokeza katika nchi ... Ukweli Umezaliwa na Bikira
Maria "(Zab 84:13 ) Veritas de terra orta est!" Papa ameendelea kusema, katika
Ibada ya Noel, Siku Kuu tunayo sherehekea kila mwaka, kwa ajili ya kutimizwa kwa
unabii: 'ukweli ulio jichomoza katika nchi, na haki kuangalia chini kutoka mbinguni'.
Ukweli, ambayo ni kiini cha Baba, umejitokeza duniani , kupitia tumbo la mama. Ukweli
unaotawala dunia, umechipuka duniani, na kushikwa katika mikono ya mwanamke ...
Ukweli ambayo mbingu haziwezi kuuzuia, umejichomoza katika nchi, na na kulazwa horini.
Je ni kwa faida ya nani Mungu Mkuu, kuwa hivyo mnyenyekevu? Hakika si kwa faida
yake mwenyewe, lakini kwa faida yetu kubwa, iwapo tunaamini.
"Kama tunaamini,
tutaiona nguvu ya imani . Mungu ametimiza kila kitu; amefanya hata lisilo wezekana
, kuwa mwili. Uweza wake wote Mkuu wa upendo , umekamilisha jambo linalo pita ufahamu
wote wa binadamu , milele kuwa mtoto na kuingia katika familia ya binadamu. Na bado,
Mungu huyo , hawezi kuingia ndani ya moyo wangu kama sita mfungulia mlango. Porta
fidei! mlango wa imani! Tunaweza kutishwa na hili , kutokana na udhaifu wetu wa kibinadamu.
Kwa ubiandamu, kufungamana na Mungu, inaweza kutuogofya. Lakini kwa kuona hali halisi,
hukimbiza mbali hofu na kuwa na tumaini linaloshinda woga. Kweli imejitokeza! Mungu
kazaliwa. Nchi imezaa matunda (Zab 67:7). Ndiyo, kuna ardhi nzuri, ardhi yenye
rutuba, nchi iliyo huru katika yote, ubinafsi na ukosefu wa uwazi wote. Katika ulimwengu
huu kuna udongo mzuri ambao Mungu aliuandaa, ili apate kuja kukaa miongoni mwetu.
Makao ya uwepo wake katika dunia. Hii nchi nzuri, ipo hata leo, mwaka huu 2012, kutoka
nchi hii , ukweli umejitokeza. Hivyo, kuna matumaini katika dunia, matumaini tunayo
weza kuamini, hata katika nyakati ngumu sana na katika hali ngumu zaidi. Ukweli umezaliwa
kwa ajili ya kuleta matumaini , wema, haki na amani.
Papa ametolea sala yake
ili amani iweze kujichipuka kwa watu wa Syria, ambao mioyo yao imepondeka na migawanyiko
inayosababishwa na mizozo isiyojali hata watu wanyonge wasioweza kujitetea wenyewe
na kuvuna waathirika wasio na hatia. Kwa mara ingine Papa ametoa ombi kwa wahusika
wote kusitisha umwangaji huo wa damu , na kuruhusu pia huduma na misaada kuwafikia
wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao ya kudumu . Papa Pia amewaomba wanasiasa
waketi chini pamoja ili kupata ufumbuzi wa kisiasa unafaa kusitisha mgogoro huo.
Amani
na ichomoze katika Nchi ambapo Mkombozi alizaliwa, na kuwapatia Waisraeli na Wapalestina
ujasiri mkuu, kumaliza migogoro na migawanyiko ya miaka mingi, na ili waweze kutembea
katika njia ya majadiliano.
Na kama ilivyo katika mataifa ya Afrika ya Kaskazini,
ambako tunashuhudia , hatua kubwa katika mapito kwa ajii ya hali ya siku zijazo ,
na hasa kwa taifa pendevu la Misri , lililo pata kubarikiwa na utoto wa Yesu – Watu
na waweze kufanya kazi kwa ushirikiano na mshikamano , kwa ajili ya kujenga jamii
iliyosimikwa katika misingi ya haki na heshima kwa uhuru na hadhi ya kila mtu.
Amani
na ichupuke katika bara kubwa ya Asia. Mtoto Yesu na alitazame kwa macho yake ya
neema, wakazi wa nchi hizo na, kwa namna ya pekee, kwao wote wale wanao mwamini Yesu.
Mfalme wa Amani, na awageukie viongozi wapya wa Jamhuri ya Watu wa China ambao majukumu
makubwa yanawasubiri. Ni matumaini yangu kwamba, wataweza kutimiza kazi hii, kwa
namna ambamo wanaweza kusaidia kujenga jamii ya kidugu kwa manufaa ya watu wote wa
taifa heshimiwa la China na duniani kote.
Kuzaliwa kwa Kristu na kuwezeshe
kurudisha amani Mali na mapatano nchini Nigeria, ambako ukatili wa kighaidi, unaendelea
kuvuna waathirika, hasa miongoni mwa Wakristo. Pia Mkombozi aweza kuwa msaada na faraja
kwa wakimbizi kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na amani nchini
Kenya, ambako kumekuwa na mashambulizi ya kikatili kwa raia na katika maeneo ya kuabudu.
Mtoto
Yesu na abariki idadi kubwa ya waamini wanao shereheka naye katika mataifa ya Amerika
Kusini. Na awaongezee fadhila za kuthamini binadamu na tunu za kikristo, zidumu kwa
wale walazimishwa kuondoka au kuwa mbali na familia zao na nchi yao, na pia awaimarisha
viongozi wa serikali katika dhamira yao ya kufanikisha maendeleo kw awote na kukomesha
uhalifu.
Papa amekalisha ujumbe wake akisema, Ndugu zangu, wake kwa waume!
Wema na ukweli, haki na amani vimekutana, na kumwilishwa ndani ya Mtoto aliyezaliwa
na Maria,horini Bethlehemu. Mtoto huyo ni Mwana wa Mungu; Mwana wa Mungu anaye
onekana katika historia. Kuzaliwa kwake, ni kuchanua kwa maisha mapya kwa ajili ya
binadamu wote. Naomba kila nchi, iwe nchi nzuri yenye kupokea na kufadhili wema na
ukweli, haki na amani. Heri ya Krismasi kwenu nyote!