Katika adhimisho la Jumapili ya nne ya Majilio, Wadomenikani duniani kote, walifanya
kumbukumbu ya mahubiri ya kihistoria, yaliyokemea na kulaani vikali ukosefu wa Haki
katika Jamii, hasa yakilenga kwa watu mahalia,walio porwa haki ya utu wao na maisha
huru ya kiutu na utulivu. Mahubiri hayo yalitolewa mwaka 1511 katika kisiwa
cha Hispaniola, ambayo kwa sasa inajulikana kama taifa la Haiti na Jamhuri ya Dominika