Askofu Kukah amekemea wanasiasa wanaotaka kupandia ngazi kupitia mgongo wa dini. Na
kwamba kuwa kiongozi bora si kisomo, bali yule anayetunza uaminifu na uwajibikaji
kazini. Askofu Mathew Kukah wa Jimbo la Sokoto, Kaskazini mwa Nigeria, alieleza
hilo , huku akiwashutumu wanasiasa wanaotafuta kutumia dini kuharibu eneo la Kaskazini
kwa manufaa yao binafsi. Hayo aliyatoa katika mahubiri yake wakati wa Ibada iliayosomwa
kwa ajili ya mtu mashuhuri katika eneo hilo Marehemu Yakowa.