2012-12-22 08:26:09

Waamini walei Injilisheni kwa kuyatakatifuza malimwengu!


Askofu Beatus Kinyaiya wa Jimbo Katoliki Mbulu, Tanzania, ni kati ya Mababa waliohudhuria Sinodi ya Maaskofu juu ya Uinjilishaji Mpya iliyohitimishwa hivi karibuni hapa mjini Vatican. RealAudioMP3

Katika mahojiano maalum na Radio Vatican anasema kwamba, Viongozi wa Kanisa wanaendelea kuhimizwa kutoa majiundo makini kwa waamini walei ili waweze kushiriki kikamilifu katika maisha na utume wa Kanisa.

Wakati umefika kwa waamini Barani Afrika kujivunia dhamana waliyojitwalia kwa njia ya Sakramenti ya Ubatizo, kwa kutoka kimaso maso kwenda sehemu mbali mbali za maeneo yao kumtangaza Kristo, lakini zaidi kumshuhudia kwa njia ya maisha yao adili na manyofu. Vyama vya kitume visaidie harakati za Kanisa katika azma ya Uinjilishaji Mpya, kwa kuwashirikisha waamini wengine karama na malengo ya vyama hivi.








All the contents on this site are copyrighted ©.