2012-12-22 12:31:25

Mheshimiwa Padre Estanislau Marques Chindekasse ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Dundo, Angola


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita amemteua Mheshimiwa Padre Estanislau Marques Chindekasse, SVD kuwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Dundo nchini Angola. Askofu mteule alizaliwa tarehe 18 Agosti 1958, Huambo, Angola. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, alipadrishwa tarehe 22 Novemba 1987. Tangu wakati huo ametekeleza utume wake nchini DRC, Angola na Roma kwa ajili ya masomo ya juu alikojipatia shahada ya Uzamivu katika Falsafa.

Jimbo Katoliki la Dundo lilizinduliwa kunako mwaka 2001 na sehemu ya Jimbo kuu la Saurimo. Kwa sasa lina jumla ya Parokia 7 zinazohudumiwa na Mapadre 10: Kati yao kuna Mapadre watatu wa Jimbo na Mapadre wengine Saba ni kutoka katika Mashirika ya Kitawa. Jimbo lina jumla ya watawa wa kike 17 na Waseminari 6. Jimbo Katoliki Dundo lilikuwa wazi baada ya Askofu Josè Manuel Imbamba kuteuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Saurimo.







All the contents on this site are copyrighted ©.