2012-12-18 07:36:20

Mapadre ni manabii na askari wa Kristo wanapaswa kuwa tayari kutekeleza utume wao bila ya kujibakiza na kamwe wasimezwe na malimwengu!


Askofu mkuu Yuda Thadeus Ruwaich wa Jimbo Kuu la Mwanza, Tanzania, katika makala iliyopita alitafakari kuhusu heshima na madai ya Manabii. Leo katika mwendelezo wa makala iliyopita anagusia kwa undani zaidi kazi ya Nabii katika Ulimwengu mamboleo, kazi inayoendelezwa na Mapadre wanaoshiriki ukuhani wa Kristo bila hata mastahili yao. RealAudioMP3

Hawa ndio wanaoendelea kutoa mwaliko kwa waamini kutubu na kumwongokea Mungu, ili waweze kuonja huruma na upendo wake usiokuwa na kifani uliopelekea hata akamtuma Mwanaye wa Pekee, yesu Kristo kuja ulimwenguni kumkomboa mwanadamu kutoka katika utumwa wa dhambi na mauti.

Askofu mkuu Ruwaichi anasema, Mapadre ni Askari wa Kristo wanaopaswa kuwa tayari wakati wote kutekeleza yale yanayomhusu Mungu na Kanisa lake, kamwe wasimezwe na malimwengu wakapoteza dira na mwelekeo wa maisha na utume wao katika ulimwengu.







All the contents on this site are copyrighted ©.