China na Vatican watiliana sahihi mkata wa ushirikiano katika sekta ya elimu ya juu
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imetiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika
masuala ya kitamaduni na Vatican, tarehe 17 Desemba 2012. Pande hizi mbili zimebadilisha
hati za makubaliano yaliyoridhiwa na pande hizi mbili.
Baraza la Kipapa la
Elimu Katoliki litashirikiana na Wizara ya Elimu ya Serikali ya China katika masuala
ya elimu ya juu pamoja na kutambua rasmi vyeti na shahada zinazotolewa na taasisi
za elimu ya juu zinazomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa nchini China.
Juhudi
hizi zilifanywa na hatimaye kutiwa sahihi na Kardinali Zenon Grocholewski, Mwenyekiti
wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki na Dr. Wu Ching-ji, Waziri wa Elimu nchini China,
hapo tarehe 2 Desemba 2011 na hatimaye kupitishwa na Bunge kwa kauli moja tarehe 20
Novemba 2012.