2012-12-15 15:20:42

Roho Mtakatifu na aongoze juhudi za Uinjilishaji mpya barani Afrika, ombi la Kardinali Filoni


Kardinali Filoni akutana na Maaskofu Katoliki wa Uganda, Jimboni la Arua. Jumamosi hii, Kardinali Fernado Filoni , kama mjumbe wa Papa , katika sherehe za Jubilee ya miaka mia ya ukristu katika jimbo Katoliki la Arua, amekutana na Maaskofu Katoliki wa Uganda.
Hutoba yake kwa Maskofu , ililenga zaidi kutoa shukurani kwa kazi kubwa zilizofanywa na wamisioanri wa kwanza katika eneo la Arua , akisema kwa hakika walipanda mbegu nzuri na katika udogo mzuri wa eneo hilo, ambayo ilichanua na kuonyeshwa ukomavu wa imani, iliyowaweza kuwapa ushupavu wa kuiishi, na kuishuhudia Injili , hata katika kifo.
Alikiri kwamba, mafanikio ya imani Katoliki yanayoonekana katika eneo hilo la Kaskazini, inatokana kwa kiasi kikubwa na majitoleo ya kishujaa na bila kujibakiza kwa vizazi vingi ya wamisionari, walio fika katika eneo hilo , kumshuhudia Kristo. Na bila ya kuchoka watu hawa wa kujitolea na wake kwa waume, mpaka leo hii umahiri wao, bado unaonekana, katika udongo wa mkoa huo, na Afrika kwa ujumla.
Na hivyo waamini wa nyakati hizi, inakuwa ni deni kutoa shukurani na fadhila, kama alivyoeleza Papa Paulo VI, Katika homilia yake kwa ajili ya Misa, iliyohitimisha Kongamano la Maaskofu wa Uganda mjini Kampala Julai 31, 1969. Alibainisha: "Kwa sasa, Waafrika ni wamisionari wenyewe. Kanisa la Kristo, ni vizuri na kwa kweli, limepaswa kupandikizwa katika udongo huu tukufu.
Kardinali Filoni, amekumbusha moja ya wajibu unaotakiwa kutimizwa ni kukumbuka wahenga na hata leo , waliowahubiri Injili; kama Maandiko Matakatifu yanavyo onya 'kumbuka viongozi wenu, wale ambao waliongea na nanyi Neno la Mungu; kufikiria matokeo ya maisha yao, mkaige imani yao '(Ebr 13:07). Hiyo ni historia ambayo hatupaswi kusahau, na inatoa alama ya uhalisia na heshima ya Kanisa kuwa la 'kitume'. Hiyo ni historia, inayoonekana sasa kama mchezo wa kuigiza wa upendo shupavu na majitolea ya sadaka, yanayo lifanya kanisa barani Afrika, kukua katika asili yake ya utakatifu. "
Na alitoa wito wa Papa kwa Mababa wa Sinodi iliyofanyika kwa ajili ya Afrika, ambao pia walirudia kutaja heshima zao kwa wamisionari waliopeleka neno la Injili kwa watu wa Mungu, waliofanyakazi pamoja na wenzi wao kama wamisionari, hasa kama makatekista na Watafsiri (taz. Ecclesia katika Afrika, n. 36 ).
Na ametoa shukurani zake za dhati kwa ndugu zake Maaskofu, kama mawakala kwanza wa Uinjilishaji Mpya, katikati ya changamoto zinazo wakabili mbele yao, wameendelea kujibidisha kila mmoja wao, katika shughuli za kichungaji, kitume, na kijamii , bila kuchoka au kukatishwa tamaa, katika kulijenga Kanisa katika mkoa huo. Katika kila jitihada kuhakikisha kwamba, wanakuwa ni vyombo halisi katika ufanisi wa wokovu wa watu, kwa ushirika wa kiKanisa katika ulimwengu wa maisha ya kijamii.
Kardinali alihitimisha hotuba yake , na wito wa umoja na mshikamano kwa ajili ya kufanikisha kazi za Uinjilishaji wa Watu, zilizo dhaminishwa kwao na Kanisa Katoliki Uganda, chini ya usimamizi wa Mama Bikira Maria, Mama yetu na Malkia wa Uinjilishaji. Na aliomba nguvu ya Roho Mtakatifu, ziongoze katika Utume kwa mataifa ya Afrika na kwa manufaa ya Kanisa Afrika na hasa kwa Makanisa ya Uganda.
Alirudia maneno ya Baba Mtakatifu Benedikto mwenyewe :"Inuka, Kanisa Afrika, Familia ya Mungu, kwa sababu unaitwa na Baba wa Mbinguni, ambaye wahenga wa baba zenu, walimtambua kuwa Muumba, kabla ya kuijua huruma na ukaribu wake , uliofunuliwa na Mwana wake wa pekee, Yesu Kristo" (Papa Benedict XVI , homilia, Misa Mwisho wa Sinodi ya Pili Maalum, kwa ajili ya Afrika, Oktoba 20, 2009).








All the contents on this site are copyrighted ©.