"Heri Wapatanishi", ni msisitizo wa Papa katika ujumbe wake kwa ajili ya Siku ya Amani
Duniani.
Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa ajili ya siku ya Dunia ya Amani , unasisitiza Wajibu
wa kuleta amani, na unahamasisha heshima kwa maisha ya binadamu Kardinali Peter
Kodwo Appiah Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Haki na Amani pamoja na
Askofu mkuu Mario Toso, katibu wa Baraza hili, Ijumaa waliwasilisha Ujumbe huo wa
Papa Benedict XVI kwa ajili ya Siku 46 ya Amani Duniani, adhimisho litakalo fanyika
tarehe Mosi Januari 2013. Ujumbe, emelenga katika mandhari ya tukio hili la kila
mwaka: "Heri wapatanishi,". Akiwasilisha ujumbe huo, Kardinali Turkson, alisema,
kwanza inaweza kuonekana Kuwa ujumbe wa kinadharia, lakini yaliyotajwa, ndizo hali
halisi zinazotendeka, katika ukweli. "Ni wazi unaonyesha majukumu ya kuleta amani,
ni lazima kulinda na kutetea heshima ya utu na 'maisha ya binadamu katika ukamilifu
wake na katika vipimo vyote ya binadamu, ambamo huchota uangalifu wote makini na
dharura za kupata suluhu kwenye matatizo kama vile maono sahihi wa ndoa, vipingamizi
katika haki , uhuru wa dini, masuala ya kazi na ukosefu wa ajira, mgogoro wa chakula,
mgogoro wa kifedha, na jukumu la familia katika elimu. Hivyo ujumbe wa Papa ,
unatoa wito wa kuwa na mtindo mpya wa kiuchumi na kusitisha udikteta wa imani kwamba
, maarifa na maaadili ni mambo ya mpito yanayotawaliwa na uwezo wa akili ya binadamu
na wakati. Papa anatoa ujumbe wake kama muhtasari mfupi wa Mafundisho Jamii ya
Kanisa na mwongozo kwa Wakatoliki , kwa ajili ya ushiriki wa kijamii na kisiasa.
Papa anatualika kuziishi heri nane za Injili, kwa ajili ya kujenga jamii yenye kuzingatia
ukweli, uhuru, upendo na haki. Papa anawaasa wale ambao wameishikila imani kwa
Mungu na ahadi zake, huweza kuuona ukweli. Na kinyume chake, wale wasiokuwa na imani
kwa Mungu, hujishaua wenyewe kwa kufanya mikakati yao ya binadamu, yenye kuwakosesha
kuuona ukweli . Bila Mungu, kwa kweli, hatima yake daima ni kutawaliwa na nguvu
za kutaka faida, na hukaribisha mifumo yote ya dhambi : ubinafsi na ukatili, uchoyo
na tamaa ya madaraka na utawala, kutovumilia, chuki na kudhulumu miundo. Maelezo
ya Papa, yanaonyesha kwamba, Amani ni sharti la kuvunja udikteta wa nadharia ya kufikiri
kwamba, maarifa na maaadili ni mambo ya mpito yanayotawaliwa na uwezo wa akili ya
binadamu. Mawazo hayo potofu katika dhana ya maadili ya uhuru kamili huzuia utambuzi
muhimu wa asili ya maadili ya sheria iliyoandikwa na Mungu ndani ya dhamiri ya kila
mtu. " Tu katika njia hii amani inakuwa inawezekana tena kuachana na doto hizo za
amani ya bandia. Amani ya kweli ni "karama ya Mungu kwa mwanadamu." Amani Ni pamoja
na Mungu, amani kwa mwenyewe, amani na mtu mwingine na kwa viumbe wote. Papa anapendekeza
mfumo mpya wa kiuchumi, uachane na nadharia za kutaka faida za harakaharaka kwa ajili
ya manufaa binafsi lakini kutathmini hali za watu, katika uwezo wao wa kukidhi mahitaji
licha ya ushindani. Mfumo mpya wa kimaendeleo uliosimikwa katika msingi wa udugu
na kugawana, ufadhili na mantiki ya zawadi: ili kwamba kila mmoja ajisikie ni wajibu
wake kujali mahitaji ya wengine, kwa kushirikiana na wengine katika mali zao. Ni
kuuvua moyo wa ubinafsi,na kutambua kwamba katika kuwa daima na Mungu, binadamu anakuwa
familia moja. Papa ameendelea kutazama utendaji kwa ajili ya manufaa ya familia
na haki ya kijamii, na dhamira ya elimu yenye faida ya kijamii akisema, ni muhimu
kukuza na kueneza "mawazo, maneno na matendo ya amani"yaliyo jengwa katika mawazo
na utamaduni wa amani, uaminifu, heshima, na urafiki. Haja kufundisha watu maana
ya upendo na kuelimisha juu ya amani, na kuishi pamoja na wema katika hali za kuvumiliana.
Na pia kuwa walimu wa kutoa msamaha, na katika kujikatalia ulipizaji wa kisasi.
Kuushinda ubaya kwa wema, na kuwa na" huruma, mshikamano, ujasiri na uvumilivu "Yote
haya – Papa anasema si ndoto za kufikirika, lakini ni "polepole, yanakuwa ni mageuzi
ya kiroho, elimu na maadili ya juu na dira mpya ya historia ya binadamu." "Kanisa
- amesema Papa – lina amini kuna haja ya kumtangaza upya Yesu Kristo, kwa sababu,
kwanza, ni mkuu wa maendeleo kamili ya watu na pia ya amani." "Alama ya amani, kulingana
na neema ya Yesu, ni moja ya sifa za atafutaye , maisha makamilifu ya kiroho na kimwili,
leo na kesho”