Ujumbe wa Papa kwa Siku ya Amani Duniani, umewasilishwa
Ijumaa hii katika ukumbi wa Yohane Paulo 11, ndani ya jengo la habari la Vatican
, kulifanyika Mkutano kwa wanahabari, kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe wa Papa Benedikto
XV1, kwa ajili ya adhimisho la 46 la Siku ya Dunia ya amani. Maadhimisho yanayofanyika
kila mwaka tarehe Mosi January. Ujumbe wa Papa unaongozwa na Mada : Heri wapatanishi.
Kati ya walioongoza uwasilishaji wa ujumbe huo ni pamoja na Kardinali Peter
Kwodo Appia Turkson , Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Haki na Amani. Pia Askofu
Mkuu Mario Toso , Katibu wa baraza la haki na amani , na pia Flaminia Giovanelli
, Katibu mwanandamizi katika baraza hilo . Kardinali Turkson, akitoa maelezo katika
mkutano huo amesema, kufuatia muonekano wa Baba Mtakatifu katika mtandao wa Twitter,
imeonekana kuwa ni njia nzuri inayofaa zaidi katika kukutana na waandishi wa habari
wengi zaidi, kuliko yalivyo mazoea ya kukutana ana kwa ana na wanahabari.
Papa
kwa ajili ya adhimisho la Siku hiyo, amechagua kutafakari, moja ya Heri nane, za
Hotuba ya Yesu ya Mlimani: "Heri wapatanishi. Kardinali anasema, "Ujumbe huo, unafungua
wito mpya katika tukio la kustajaabisha katika maisha ya Kanisa, ambao ni Mtaguso
Mkuu wa Pili wa Vatican, ambao hivi karibuni Mama Kanisa, alifanya maadhimisho ya
kutimia miaka 50 ya uwepo wake. Ni tukio linaloonyesha nguvu ya utume wa kanisa
katika ulimwengu na majitoleo ya ya Wakristo katika historia ya mwanadamu .. Heri
ya kiinjili na amani kama zawadi ya Mungu kwa mwanadamu, licha ya hali za kutisha
katika ulimwengu wa utandawazi.