2012-12-14 15:18:04

Kardinali Filoni akutana na Mapadre wa Arua- Uganda


Akiendelea na ziara yake, kwa ajili ya maadhimisho ya miaka mia tangu Ukatoliki kuingia Jimboni Arua, Kaskazini mwa Uganda , Ijumaa hii, Kardinali Filoni alikutana na Mapadre na watawa wa Jimbo la Arua .

Hotuba yake , iliwasisitizia wahudumu wa kanisa kwamba, uwepo wao hapo ni uwakilishi mkubwa wa Mapadre wote, na watawa wake kwa waume, katika nchi pendevu ya Uganda. Na kwamba, wao ni washirika wa karibu wa Maaskofu katika huduma yao ya kichungaji. Na wapo katika kila eneo la maisha ya Kanisa, na matazamio ya ujio wa Ufalme wa Mungu - ufalme wa haki, upendo, na amani.

Na kwamba, kwa njia ya maombi na kazi, katika maisha yao na katika kusoma historia ya Kanisa katika nchi hii: historia ya imani kali, ya upendo na majitoleo ya sadaka,, Kardinali aliutambua mchango wa Mapadre na Wamisioanri waliosaidia kuiimarisha Jumuiya Katoliki ya Arua. Uwajibikaji wao kwa sababu ya kueneza Injili mara nyingi , wameonekana kuongozwa na ushujaa wa ajabu na hata baadhi yao kuwagharimu maisha yao, na kuwa kielelezo kwa mara nyingine kwamba, "damu hiyo ya mashahidi ni mbegu ya Ukristu katika eneo hili ", kama ilivyoelezwa katika waraka wa (Tertullian, cf. Africae Munus, 113. ).

Aliendelea kuwataka ndugu zake katika Kristo, kama makuhani, kwamba wanapaswa kutambua siri ya neema katika maisha yao ya kipadre na kitawa. Kama Mtakatifu Paulo anavyosema, wanahazina hii katika vyombo vya udongo (2 Kor 4:01.) Ni zawadi. Ni tendo la uaminifu kwa upande wa Kristo, ni wito kwao kuwa "mawakili wa siri za Mungu" (1 Kor 4:01.). "Ukuhani ni zawadi kwetu, lakini, katika wao na kupitia kwao, Ukuhani inakuwa ni zawadi kwa Kanisa".
Na aliwatazamisha katika tafakari za nusu karne, tangu uzinduzi-Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, katika umuhimu kutambua kwamba, miaka hamsini iliyopita, Maaskofu wazawa wa Afrika walikuwa wachache, licha ya mapadre na watawa Lakini leo hii katika kulinganisha, asilimia tisini ya wahudumu wa Kanisa Afrika, Maaskofu, mapadre na watawa ni wana wa Afrika. Hivyo, Kanisa sasa limekabidhiwa katika mikono na nyoyo za wana wa Afrika

Kardinali Filoni ameeeleza na kuwataka Mapadre wa Afrika kudumisha uaminifu katika ahadi zao za kikuhani na kanisa kwa ujumla ili waweze kupata mavuno mengi zaidi kwa ajili ya ufalme Bwana Yesu Kristu. Matumaini yao na yajengwe kwa Mungu aliye Hai kwelikweli.









All the contents on this site are copyrighted ©.