Papa akutana na Mabalozi wapya:ahimiza vijana kupata elimu si tu elimu dunia lakini
pia muhimu kupata elimu ya kiroho.
Leo zaidi ya siku za nyuma, vijana wana haki ya kuelimishwa hisia za uwajibikaji na
majitoleo, na serikali zinapaswa kutoa uhuru kamili katika elimu na katika kuwa mfano
mzuri wa utendaji wa haki. Ni maoni ya Baba Mtakatifu Benedikto XV1, kwa mabalozi
wapya, wakati wakiwasilisha hati za utambulisho, Alhamis hii mjini Vatican. Mabalozi
wapya wametoka Jamhuri ya Guinea, Niger, Zambia, Thailand, Sri Lanka na visiwa vya
Saint Vincent na Grenadini, Magharibi mwa Indies.
Papa aliwashukuru kwa salaam
za matashi mema kutoka kwa Marais na wakuu wa serikali wa nchi walizotoka, na pia
kwamba wameteuliwa na kutumwa kwake, kwa ajili ya kutimiza majukumu yao, katika utumishi
kwa manufaa ya watu wao. Aliwaombea Baraza zote za Mwenyezi Mungu ziwashukie wao na
wafanyakazi wenzao ili waweze kufurahia maisha ya amani na kuheshmiana wakiwa wameungana
katika umoja hapa Roma. Hotuba ya Papa kwa Mabalozi hao, ikitazama changamoto
nyingi za wakati wetu, imebaini kwamba, elimu inashika nafasi ya ya kwanza katika
umuhimu. Na imetaja mchanganyiko wa katika dunia ya sasa ya utandawazi kwamba ni
hali inayosababisha mabadiliko katika maisha na maarifa, na hivyo ikujenga uwezekano
mkubwa wa mifarakano kibinadamu, kiutamaduni, kijamii na kiroho, na mno katika historia
ya mwanadamu. Papa ameitaja familia kuwa ni kituo cha kwanza cha kutoa elimu
ya kuonekana iwapo itapandikizwa vyema akilini mwa watoto, kama msingi na asili
inayopaswa kuendelezwa daima na kizazi kipya katika maana ya uwepo wao duniani. Aidha
ni vivyo hivyo , katika maeneo ya elimu na mamlaka ya kielimu, ambamo walimu na wahadhiri,
wanapaswa kuwa kioo cha ustaarabu na maisha adilifu. Papa ameonyesha masikitiko
yake kwamba, “ kwa bahati mbaya, umahiri wa baadhi yao umekuwa si kama wanavyotazamiwa,
kwani kumekuwa na mwelekeo wa kuufinyanga ukweli na kutoa upendeleo fulani, hivyo
kukosesha ufahamu halisi licha ya kuondoa au kupunguza ukweli kuhusu binadamu.
Papa anakumbusha binadamu ni kiumbe muhimu, aiyeweza kuchukuliwa kijuujuu tu , kama
mambo ambayo yanayoweza kuchezewa kama taka. Papa ameasa, haki ya maadili ya
elimu, kamwe isipuuzwe au kukataliwa. Na Wajibu ya kuelimisha maadili haya kamwe
yasimezwe au kudhoofishwa na maslahi yoyote ya kitaifa au itikadi na kisera. Papa
ameitaja hiyo ndiyo sababu msingi ya kwa nini ni muhimu kuwaelimisha vijana katika
ukweli na ukweli. Papa alimalizia hotuba yake kwa kuwaweka chini ya usimamizi wa Mama
Bikira Maria , Mama wa Waheshimiwa wote. Na kwamba, idara za Jimbo Takatifu Curia
ya Roma, zitakuwa wazi daima kutoa msaada kwao kila wanapohitaji. Na kwa furaha aliwapa
baraka zake za kipapa wao na familia zao.