Umoja wa Wakristu ni maluwiluwi au ahadi?:Matumaini ya Kiekumene katika mwaka wa
Imani. Ni mada iliyoongoza Mhadhara wa Jumatatu katika Chuo Kikuu cha Lateran cha
Roma. Mhadara huo uliogozwa na Mwanateolojia Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza
la Kipapa kwa ajili ya uhamasishaji wa Umoja wa Wakristu .
Katika tafakari
yake, Kardinali Koch alisisitiza umuhimu wa kudumisha lengo la umoja kamili, lenye
kuonekana kwa Makanisa kama njia pekee ya kutoa ushahidi wa kuaminika wa imani ya
kikristo katika jamii ya leo, inayomezwa na mambo ya kidunia.
Kardinali Kuch
akirudi katika madhari hii iliyojadiliwa hivi karibuni katika Mkutano wa Mwaka wa
Baraza lake, alitaja tena umuhimu wa ekumeni katika moyo wa uinjilishaji wote mpya,
kupambana na wazo la kisasa la malimwengu na ubinafsishaji wa dini, akibainisha kama
sehemu ya matokeo ya kutisha ya mgawanyiko na migogoro michungu kati ya Makanisa
ya karne ya 16 na 17.
Aliendelea kueleza, tangu Mkutano wa kwanza wa Dunia
ya Kimisionari, uliofanyika Edinburgh mwaka 1910, imezidi kujionyesha kwamba, utoaji
wa ushuhuda wa kweli wa Injili ya Kristu, utafanikishwa veyma zaidi iwapo Makanisa
yataweza kuondoa utengano uliopo na kutembea pamoja kama wamoja.
Kardinali
Koch pia alisisitiza umuhimu sala katika kutafuta umoja Wakristu: kama Yesu alivyoomba
katika karamu ya mwisho alipokuwa na wanafunzi wake "na wawe wamoja ili kwamba, ulimwengu
upate kuamini". Kwa njia hiyo, Wakristu wote leo hii, wanapaswa kuongozwa na yote
mawili sala na ushuhuda wa matendo, kupitia njia ya mapatano na umoja kamili wa
Mwili Mmoja wa Kristo.