2012-12-11 14:38:56

Askofu mkuu Paul Richard Gallagher ateuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Australia


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Askofu mkuu Paul Richard Gallagher kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Australia. Kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Guatemala.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Paul Richard Gallagher alizaliwa tarehe 23 Januari 1954. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 31 Julai 1977. Tarehe 13 Machi 2004 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu. Katika maisha yake amefanya utume wake kama Balozi wa Vatican nchini Burundi na Guatemala.







All the contents on this site are copyrighted ©.