Umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa kushirikiana kwa pamoja ili kupata suluhu ya kudumu
Ukanda wa Sahel, Kaskazini mwa Afrika
Professa Roma Prodi, mwakilishi maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwenye
Ukanda wa Sahel, Kaskazini mwa Afrika, hivi karibuni alitembelea na kufanya mazungumzo
na maafisa waandamizi kutoka Umoja wa Mataifa wanaowakilisha mashirika mbali mbali
katika ukanda huu, ili kuzungumzia kinzani zinazoendelea sehemu hizi.
Kwa
pamoja wamejadili matatizo msingi yanayoukabili Ukanda wa Sahel na jinsi ya kukabiliana
na changamoto hizi kwa kuunganisha na kuimarisha nguvu zao za pamoja ili kuhakikisha
kwamba, misingi ya haki, amani na utulivu inadumishwa. Wamefanya upembuzi yakinifu
kuhusu hali tete nchini Mali na jinsi ambavyo Jumuiya ya Kimataifa inavyoweza kuchangia
katika mchakato wa kupata suluhu ya kudumu.
Kwa pamoja wamebainisha umuhimu
wa kushirikiana ili kuweza kupata ufumbuzi wa kudumu wa migogoro iliyopo kwenye Ukanda
huu, ili hatimaye, wananchi waweze kufurahia maendeleo endelevu.