2012-12-10 15:06:04

Mwandalieni njia Emmanuel- Papa


Jumapili, licha ya baridi iliyokuwepo katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, maelfu ya watu walikusanyika katika uwanja huo nyakati za mchana kusikiliza hotuba ya Papa na kusali pamoja nae sala ya Malaika wa Bwana .
Katika hotuba yake, Papa alihimiza waamini kuiandaa mioyo yao na maisha yao ya kila siku, kwa ajili ya ujio wa Bwana , kama alivyo himiza Yohane Mbatizaji katika Injili ya Luka.
Aliizungumzia sauti iliayo nyikani, akisema, leo hii inaililia jamii ya ulaji , inayopendelea kujilimbikizia mali na vitu vya anasa, na kujifurahia maovu, badala ya kumcha Mungu na kuzishika amri zake, . Kilio cha Yohane Mbatizaji jangwani, kinafundisha watu kuishi kwa njia inayofaa , ili kwamba kipindi cha Noeli, isiwe tu kipindi cha furaha za nje , lakini furaha ya ndani ya moyo, furaha ya kumpokea Mwana wa Mungu , mwenye kuleta furaha na amani ya kweli kwa wanao mwamini.








All the contents on this site are copyrighted ©.