2012-12-10 14:51:34

Kanisa lahitaji mchango thabiti wa Waamini, Papa asisitiza ema..


Kanisa la Ulimwengu linatazamia na linahitaji moyo wa Kitume, mwamko, ukarimu na mchango thabiti , usiokuwa na mbadala toka kwa waamini Marekani zote mbili Kaskazini na Kusini . Baba Mtakatifu alieleza siku ya Jumapili jioni wakati akihutubia Makardinali, Maaskofu, Mapadre, Watawa na walei kutoka Bara za Amerika
Umati huo ulikusanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro , Vatican, kushiriki Ibada ya Misa , kwa ajili ya Ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa juu ya Kanisa. Kongamano lililoanza Jumapili hiyo 09 -11 Desemba kwa ajili ya kuadhimisha miaka 15 tangu kufanyika kwa Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Amerika, na Mwaka wa Imani RealAudioMP3








All the contents on this site are copyrighted ©.