2012-12-10 13:34:20

Jimbo Katoliki Mbeya lapata Mashemasi Wapya sita!


Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo Katoliki Mbeya, ametoa daraja takatifu la Ushemasi kwa Mafrateri sita waliokuwa wanasoma Seminari kuu ya Kipalapala na Peramiho na Segerea baada ya kuhitimu sehemu hii ya kwanza ya majiundo yao ya Kipadre. Ibada hii imefanyika kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Anthony wa Padua, Jimbo Katoliki Mbeya.

Katika mahubiri yake, Askofu Chengula, amewataka waamini kujitosa kwa hali na mali ili kujenga Kanisa linalowategemea sana, hasa wakati huu wa maadhimisho ya Mwaka wa Imani sanjari na kumbu kumbu ya maadhimisho ya miaka 50 Jubilee ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, ambao unatoa mwongozo wa pekee kwa waamini walei kushiriki kikamilifu katika maisha na utume wa Kanisa. Umoja na mshikamano wa dhati ni matunda ya Roho Mtakatifu kwa Kanisa.

Waamini wanachangamotishwa na Mama Kanisa kujenga na kudumisha umoja, upendo na mshikamano wa dhati na wachungaji wao, daima wakiwa mstari wa mbele kutolea ushuhuda wa imani tendaji badala ya kuendekeza majungu na migawanyiko isiyokuwa na tija wala maendeleo na ustawi kwa Kanisa. Imani hii kwa namna ya pekee, ijioneshe kwa kuiungama, kuiadhimisha, kuiishi na kuisali. Waamini walipambe Kanisa kwa njia ya matendo na maisha yao adili.

Mashemasi wapya ni Karolo Betold Ilonga kutoka Seminari kuu ya Kipalapala.
Shemasi Francisko Edward Ngao kutoka Seminari kuu ya Peramiho.
Shemasi Simoni Msompa kutoka Seminari kuu ya Peramiho.
Shemasi Thomas Mwampamba kutoka Seminari kuu ya Segerea.
Shemasi Augustino Kanku Lukusa wa Shirika la Marafiki wa Kristo.







All the contents on this site are copyrighted ©.