2012-12-07 11:28:16

Mr. Georgio Papadopoulos awasilisha hati zake za utambulisho mjini Vatican


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Ijumaa, tarehe 7 Desemba 2012 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Georgios Papadopoulos, Balozi mpya wa Ugriki mjini Vatican. Alizaliwa kunako mwaka 1954, ameoa na amebahatika kupata mtoto mmoja.

Alianza shughuli zake za kidiplomasia kunako mwaka 1980. Ni mtu aliyebobea katika masuala ya kidiplomasia kutokana na kuwa na uzoefu na man'amuzi mapana, kwani tangu wakati huo wote amebahatika kufanya kadi katika nyadhifa mbali mbali ndani na nje ya nchi yake.







All the contents on this site are copyrighted ©.