2012-12-07 15:40:54

Mh. Padre Peter Ebere Okpaleke ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Ahiara, Nigeria


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Mheshimiwa Padre Peter Ebere Okpaleke wa Jimbo Katoliki Awka, Nigeria kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Ahiara. Askofu mteule alizaliwa tarehe 1 Machi 1963. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, alipadrishwa tarehe 22 Agosti 1992 kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Awka, Nigeria.

Tangu wakati huo ameteuliwa katika nyadhifa mbali mbali Jimboni mwake. Kati ya Mwaka 2002 hadi 2011 alijiendeleza kwa masomo ya juu kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Santa Croce, kilichoko mjini Roma na kujipatia shahada ya uzamivu.

Kuanzia mwaka 2011 alikuwa ni Paroko hadi anateuliwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Ahiara, kufuatia kifo cha Askofu wa kwanza Victor Chikwe, kilichotokea hapo tarehe 16 Septemba 2010.







All the contents on this site are copyrighted ©.