2012-12-07 14:55:30

Askofu mkuu Zimowksi kumwakilisha Papa kwenye Maadhimisho ya 21 ya Wagonjwa Duniani kwa Mwaka 2013


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Askofu mkuu Zygmunt Zimowski, Rais wa Baraza la Kipapa la huduma za kichungaji kwa ajili ya wafanyakazi wa sekta ya afya, kuwa mwakilishi wake maalum katika Maadhimisho ya Siku ya Ishirini na moja ya Wagonjwa Duniani, itakayoadhimishwa hapo tarehe 11 Februari 2013, mjini Altotting, nchini Ujerumani.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu kuwa mwakilishi wake kwenye Jubilee ya Miaka 50 ya Madhabau ya Bikira Maria wa Afya Njema, yaliyoko nchini India sanjari na maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 25 tangu Baraza la Maaskofu Katoliki India lilipoanzishwa. Sherehe hizi zinatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 9 hadi 11 Februari 2013.







All the contents on this site are copyrighted ©.