2012-12-06 16:01:23

Mwaka wa Imani nafasi ya kujenga moyo wa hisani- Askofu Mkuu Bader


Ili kuijenga nchi ya kisasa na kidemokrasia ni lazima kwanza kuujenga uzalendo wa raia. Askofu Mkuu Ghaleb Bader, wa Jimbo Kuu la Algiers, Algeria,ameandika katika tahariri yake, katika gazeti la “Rencontres”, toleo la Desemba.
Amebainisha kwamba, katika mwaka huu wa imani ambamo Caritas Algeria pia ina sherehekea miaka 50 ya kuanzishwa kwake nchini Algeria, inakuwa ni kipindi kwa kila mmoja, kujitahidi kujenga moyo mkarimu zaidi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watu wasio kuwa na namna za kupata mahitaji yao msingi ya kibinadamu. Na pia ni wakati wao wa kufanya jitihada zaidi kuijenga nchi kisasa na kidemokrasia.
Askofu Mkuu Ghareb anaona "Leo hii, Algeria bado haija kamilisha mradi wa kuifanya Algeria , kuwa nchi huru na kisasa. Na hivyo ametoa wito kwa Caritas Algeria, kujitoa kwa ukarimu zaidi kwa watu wa nchi hiyo , bila kujali tofauti zao za kitamaduni na kidini.
Mhashamu Askofu Mkuu Bader anasisitiza , " hakuna maendeleo n ya kweli kwa mtu binafsi na hata maendeleo ya nchi kwa ujumla, kama hakuna uhuru wa kweli. Na hakuna demokrasia au nchi ya kisasa",bila mtu kuwa huru kamili , kijamii, kimbali na kidini pia. Ameiita uhuru huo, kuwa msingi wa utume wa Kikristo na wa Kanisa ... Maana Kanisa huudhihirisha uhuru huo kupitia upendo ulionyeshwa na Kristo hadikifo cha msalabani, ni upendo kupitia matendo ya hisani na ishara ya mshikamano na udugu. "
Askofu Mkuu wa Algiers pia anasema kuwa "upendo ni rahisi kuutoa, tena kwa uthabiti kama msaada kwa jirani mhitaji, au kama jibu moja msingi katika hitaji la mtu kuuona upendo wa Mungu aliye Hai. Na huonekana na kutekelezwa kupitia matendo ya udugu na kujaliana. Ni upendo wenye kupambana dhidi ya maovu ambayo ni matokeo ya dhambi na madhara yake yote, njaa, ukosefu wa haki, vurugu, chuki, ubaguzi wa rangi .
Mons. ameendelea kuasa kwamba, katika mwaka huu ambao Algeria Caritas inasherehekea miaka 50 katika kazi zake, na Mwaka wa Imani, maadhimisho haya yana sisitiza uhusiano kati ya imani na upendo. "Pasipo imani, si rahisi kuwa na upendo wa kina kwa wengine na hasa wahitaji. Ni maadhimisho yanayokataa ubinafsi, ila kuukumbatia upendo wa kweli. Upendo si kwa kunena tu lakini wenye kuonekana kiutendaji na shuhuda za maisha , katika asili yake ya Imani ya Kikristu.








All the contents on this site are copyrighted ©.