2012-12-05 07:22:16

Baba Mtakatifu Karibu kwenye Jukwaaa la Mtandao wa Kijamii, Utwitter pamoja nasi!


Rais Shimon Peres wa Israel ni kati ya watumiaji wa kwanza wa mtandao wa kijamii Twitter kumwandikia Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, akimwalika kwa mikono miwili katika mtandao wa twitter kwa kusema kwamba, katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni uhusiano kati ya Vatican na Israel umeboreka kwa kiasi kikubwa na kwamba, kwa pamoja wanaweza kutangaza misingi ya amani.

Ujumbe wa Rais Shimon Peres umeandikwa kwenye akaunti ya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita @pontifex ambayo hadi sasa inaendelea kuzua gumzo kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Wachunguzi wa mitandao ya jamii wanasema kwamba, hadi sasa zaidi ya watu nusu millioni wamekwisha jiunga kwenye akaunti ya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita.







All the contents on this site are copyrighted ©.