Tahariri ya Padre Federico Lombardi- Saburi na tumaini la majilio
Tahariri ya Padre Federico Lombardi kwa wiki hii, imeangalishwa katika kipindi cha
majilio, kipindi cha kusubiri kwa tumaini, licha ya matatio ya kiuchumi na ukosefu
wa ajira .
Amesema , kwa mara ingine, kinaanza kipindi cha majilio, wakati
wa saburi na tumaini tunaloliangalisha katika Siku Kuu ya Noel.
Na kwamba,
dunia kamwe haikosi matatizo na hali ngumu zinazomgusa binadamu katika njia yake ya
ubinadamu na imani. Kwa mtazamo wa haraka katika mazingira yanayotuzunguka, tunaiona
hali hiyo.
Padre Federico Lombardi ameendelea kuzungumzia matatizo ya Kiuchumi
na ukosefu wa ajira, yanayorarua maisha ya watu wengi na kuwakosesha tumaini kwa siku
zijazo na kudumaza juhudi za kuanzisha miradi mipya.
Pia amegusia matatizo
ya kijamii na afya kama ilivyoelezwa katika maadhimisho ya Siku ya Kupambana na madhulumu
dhidi ya wanawake na Maadhimisho ya Siku ya Dunia ya kupambana na ukimwi. Si hivyo
tu lakini pia kuna matatizo ya machafuko ya kivita na migongano kama ilivyo huko Syria
, Mali, Nigeria, Mashariki mwa Congo, Somalia , Afghanistani, na Iraq. Pia jamii inakabiliana
na hali za mivutano na wasiwasi kijamii na kisiasa, kama ilivyo huko Misri.
Mhariri
anasema, katika hali hizo, si rahisi kuitambua taa ya matumaini, hata kama baadhi
hazikosekani, kama ilivyo katika mazungumzo yanayoendelea kati ya serikali ya Cuba,
na kati Colombia na waasi FARC, na kupigwa kwa kura juu ya Palestina na Umoja wa Mataifa,
pengine ni msukumo wa kuanza kwa mchakato wa amani na kama matumaini halali.
Padre
Federico Lombardi amekamilisha tahariri yake na maelezo kwamba, kwa kifupi, tunaishi
kati ya changamoto, wasiwasi, na matumaini tete. Hivyo kipindi cha Majilio kinapaswa
kutusaidia kujiuliza na kutafuta majibu kwa matumaini makubwa, na tusikubali kumezwa
na ukosefu wa matumaini, badala yake tujawe na tumaini ya ubinadamu, katika kipindi
hiki cha matarajio.
Padre Federico Lombardi ameweka tumaini lake katika Juhudi
zote za tafiti za kisayansi , kidiplomasia na kisiasa katika kutafuta amani ya kijamii,
ndani kitaifa na ya kimataifa, katika maana na mshikamano unaomulikiwa tu kwa kina
na uogofu wa mtu , unao mwezesha kuwa mtendaji wa amani kama alivyosema Bwana. Lakini
ili iwe hivyo , tunapaswa kuutulea muda wa kipindi hiki cha majilio katika sala na
kazi .