2012-12-01 17:18:40

Papa akutana na Wasanii na wanasarakasi wa Italia.


Jumamosi nyakati za adhuhuri, katika ukumbi wa Paulo VI wa Vatican, Papa aliwapokea wasanii na wanasarakasi wasiopungua elfu saba, ambao hufanya maonyesho yao barabarani na mitaani. Tukio lililofanikishwa kwa ufadhili wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Wahamiaji na Watu wasiokuwa na makazi maalum.

Papa akiwahutubia wasanii hao alisema, Kanisa ni hujaji kama walivyo wao. Na aliwahimiza kushirikiana katika kazi ya uinjilishaji mpya. Hotuba ya Papa ilitanguliwa na hotuba fupi kutoka kwa Kardinali Antonio Maria Veglio, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum. Pia shuhuda kadhaa na onyesho la kisanii.
Papa, alionyesha kujali kwamba, maisha yao ya kisanii, mara nyingi ndani mwake ni maisha ya kujitolea mhanga, yanayohitaji utambuzi wa kina uliosimikwa katika misingi ya maadili ya kijamii na kiroho na upendo thabiti wenye kukumbatia familia, na huduma kwa wazee , mzizi wa uzoefu wao wa mitaani.
Ustadi wao kwa kweli, Papa alisema , unahitaji fadhila na majitoleo ya kisadaka katika uwajibikaji , uvumilivu, ujasiri na ukarimu, na kutokatishwa tamaa jamii ya leo inayo onyesha pengine kutovutiwa tena na kazi yao.
Papa alionyesha kutambua mchango mkubwa katika kuunda familia thabiti kati ya vizazi, kuzisifu kwa mshikano wake wa kifamilia licha yakuwa na tabia za kuvijari vinjari safirini.

Kwenye mazingira hayo , Papa aliwasisitiza kudumisha mwendelezo makini na hai kati ya vizazi, kwa maana ya urafiki wa kweli na ladha ya kazi katiak umoja wao. .

Papa kisha, alisisitiza kuwa, hata katika ulimwengu sarakasi, kunahitajika uinjilishaji mpya na utoaji wa ushuhuda hai katika uadilifu wa Kiinjili, , hasa katika uso wa matatizo ya maisha na "majaribu ya kutoaminiana". Kanisa, aliendelea, ni "Hija kama wao wenyewe, katika dunia hii". Na hivyo wanaitwa kushiriki katika Utume wa kimungu, kupitia njia hii ya maisha yao ya kila siku.
" Papa pia alirejea matatizo mengi yanayo husiana na tabia yao ya kusafirisafiri , ikiwemo ugumu wa elimu kwa watoto kutokana na kunyimwa vibali vya uraia, kwa ugeni wao katika mataifa.

Papa alionyesha tumaini lake kwamba , serikali zitatambua umuhimu wa kazi hizi za usanii katika jamii na utamaduni, akiomba raia mahalia waondokane na roho ya chuki dhidi ya wageni. Na kwamba jamii iweza kukaa nao kwa muda mrefu, katika hali ya kirafiki na maelewano na uwezo wa kukidhi mahitaji yao ya kiroho."

Na wasisahau kwamba, familia ni njia msingi ya maambukizi ya imani." Familia yako, daima shule ya imani na upendo, ushirika na udugu."Papa alihitimisha hotuba yake.
Mwanahabari Alessandro Gisotti, akishuhudia tukio hilo amesema, kwa Vatican , ilikuwa ni mazingira ya furaha tele , hasa kwa uwepo wa kundi kubwa la watoto waliovalia kisanii ambao waliupamba ukumbi wa Paulo wa V1 kwa maonyesha ya kisanii ya kushangaza. Ilikuwa ni kulifikisha tabasamu la Vijana karibu na Papa .

Papa pia alipata fursa ya kukiona kitoto kidogo cha simba kilichokuwa kimeshikwa na mmoja wa wanasarakasi.








All the contents on this site are copyrighted ©.