Mwendo mmoja kuelekea muungano wa Kanisa, licha ya njia ndefu na ngumu - Papa
Baba Mtakatifu Benedikto XV1, kwa ajili ya adhimisho la Siku Kuu ya Mtakatifu Andrea,
Msimamizi wa Upatriaki wa Kiekumene wa Constantinople, alipeleka ujumbe wake kwa Patriaki
Bartolomeo I. Siku Kuu iliyoa adhimishwa na Mama Kanisa siku ya Ijumaa iliyopita.
Ujumbe wa Papa uliwasilishwa kwa Patriaki Bartholomeo I, na Kardinali Kurt
Koch, Rais Wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Umoja wa Wakristu, aliyeongoza Ujumbe
wa Vatican Istanbul kwa ajili ya maadhimisho ya Siku Kuu hii.
Papa katika
salaam hizo, ameonyesha , tumaini lake katika umoja wa kweli na halisi , licha kwamba
bado kukamilika, utajengwa katika misingi, si yenye harahara za nadharia za fadhila
nyepesi za kibinadamu, lakini juu ya imani moja katika Bwana Yesu Kristo."
Kwenye
ujumbe huo kwa Patriaki wa Kiekumene, Bartholomayo I, Papa amehimiza kusonga mbele
katiak hali ya kujiamini , katika njia inayolenga kurudisha, umoja kamili." Barabara
ambayo mpaka sasa imekuwa na maendeleo mengi muhimu katika kupeleka mbele hatua ,
ingawa inaweza kuonekana kuwa "ndefu na ngumu.
Kanisa Katoliki limepania kuendelea
katika mwelekeo huu –kwa kufarijiwa na sala ya Bwana wetu Yesu Kristo “aliompa Baba,
'wao pia inaweza kuwa wamoja kama wao walivyo, ili kwamba, ulimwengu upate kuamini"
(Yohana 17:21) ".
Na Patriaki Bartholomayo I, kwa upande wake katika maadhimisho
haya alisema, "njia ya kiekumeni ni haiwezi kubatilishwa," licha ya kuwa ndefu na
ngumu. Patriki aliendela alihimiza kazi za majadiliano , yanayotafuta kuonyesha manufaa
ya umoja kuliko migawanyiko.
sherehe hizi zilifanyika katika Kanisa Kuu la
Kipatriaki la Fanar, mjini Instabul.