MWAKA WA BWANA unafumbata: Mwaka wa Imani, Jubilee ya Miaka 50 ya Mtaguso Mkuu wa
Pili wa Vatican na Uinjilishaji Mpya
Mheshimiwa Padre Raniero Cantalamessa, Mhubiri wa Nyumba ya Kipapa anasema, Mama Kanisa
katika Mwaka 2012 - 2013 anaishi kwa namna ya pekee kabisa kipindi cha neema ambacho
kimegawanyika katika sehemu kuu tatu: Mwaka wa Imani uliotangazwa na kuzinduliwa na
Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita; Jubilee ya miaka 50 ya Mtaguso Mkuu wa Pili
wa Vatican; Ari na mwamko mpya wa shughuli za kimissionari mintarafu changamoto zilizotolewa
na Mababa wa Sinodi ya Maaskofu juu ya Uinjilishaji Mpya.
Katika Kipindi cha
Majilio, Padre Cantalamessa anatarajiwa kutoa mahubiri yatakayoongozwa na kauli mbiu
Mwaka wa Bwana" kama ifuatavyo: Mahubiri Awamu ya Kwanza yatakuwa hapo tarehe
7 Desemba 2012. Mahubiri Awamu ya Pili yatafanyika tarehe 17 Desemba 2012. Mahubiri
Awamu ya Tatu yatakuwa ni hapo tarehe 21 Desemba 2012.
Mahubiri ya Kipindi
cha Majilio yatagusia kwa namna ya pekee, Barua ya Kichungaji ya Baba Mtakatifu Benedikto
wa kumi na sita "Mlango wa Imani" "Porta Fidei". Yatagusa maeneo haya matatu ambayo
ni neema ya pekee kabisa kwa Mama Kanisa katika kipindi cha Mwaka huu, kweli kiwe
ni kipindi cha neema, kama ambavyo Yesu mwenyewe alitangaza Hekaluni alipokuwa anaanza
utume wake.