2012-11-30 15:19:42

Jimbo la Papa lapokea kwa mikono miwili Azimio juu ya Palestina


Jimbo la Papa limepokea maamuzi ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, yaliyo ridhia ombi la Palestina la kuwa Nchi Tazamaji katika Baraza la Umoja wa Mataifa, ingawa si mwanachama .

Jimbo la Papa, limeeza jinsi lilivyo fuatilia kwa ukaribu hatua hii lakini bila ya kupendelea upande wowote, na kwamba , limekuwa likitenda kwa mujibu wa hadhi na asili yake ya kidini na utume wake wa kilimwengu ,pia likiwa makini zaidi katika mitazamo ya uadilifu mpana katika matatizo ya kimataifa.

Jimbo la Papa , zaidi ya yote, limepokea matokeo ya kura iliyopigwa Alhamis kwa ajili ya kutoa azimio thabiti , na kwa kushirikiana na Jumuiya ya kimataifa , katika mtazamo wa azimio lililokwisha tayari ainishwa kwenye Azimio namba 181 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, la Novemba 29, 1947. Limeitaja hati hiyo kuwa hati ya msingi kisheria kwa ajili ya kuwepo Nchi mbili, moja ambayo haijawahi kusimikwa kwa kipindi cha miaka sitini na tano mfululizo , wakati taifa jingine tayari limeweza kuuoja mwanga wa uhuru.

Jimbo la Papa limeeleza na kuikumbuka tarehe 15 Mei 2009, wakati Papa Benedikto XV1, akihitimisha hija yake katika Nchi Takatifu , ambako alisema: "Hapana tena umwagaji damu! Hakuna tena mapigano! Hakuna tena ugaidi! Hakuna tena vita! Badala yake, tupanie kuvunja mduara wa vurugu. Na kuwe na amani ya kudumu yenye kuzingatia haki. Basi, na kuwe na maridhiano ya kweli na uponyaji".

Na aliitaka dunia kutambua nchi ya Israel, ina haki ya kuwepo na kufurahia amani na usalama ndani ya makubaliano ya Kimataifa . Na iwe hivyo pia watu wa Palestina pia wana haki kamili ya kuishi katika nchi yao kwa uhuru kamili na kuuishi utu wao na kusafiri kwa uhuru. Papa aliomba mataifa haya mawili yatabuliwe kihaki na isibaki kuwa ndoto.

Na kwa kuzingatia matokeo ya kura ya Alhamis, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na kwa himizo la Jumuiya ya Kimataifa, na na kwa namna ya kipekee wabia wanaohusika moja kwa moja na maamuzi thabiti ya kitendaji katika mtazamo wa kusonga mbele na malengo yaliyotajwa, , Jimbo Takatifu linapokea kwa mikono mwili maamuzi yenye neema ya Mkutano Mkuu, yanayotoa idhini kwa Palestina kuwa mjumbe mtazamaji asiyekuwa mwanachama, katika Umoja wa Mataifa.

Ni azimio la heri linalo kumbusha pia makubaliano ya Jimbo Takatifu na Chama cha “Palestina Liberation Organisation”, ya hapo Februari 15, 2000, katika lengo la kuunga mkono, utambuzi wa jumuiya ya kimataifa, uliotoa hadhi ya kipekee kwa Yerusalemu, kulinda uhuru wa dini, dhamiri, utambulisho na mapokeo ya Yerusalemu, kama mji mtakatifu, unao heshimu uhuru wa kutembelea katika maeneo yote matakatifu ya eneo hilo.








All the contents on this site are copyrighted ©.