SECAM inadhamiria kuanzisha Taasisi ya Imani, Utamaduni na Maendeleo!
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM, katika Warsha
iliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam, kwa kushirikiana na Baraza la Kipapa
la Utamaduni, imeamua kuanzisha Taasisi ya Imani, Utamaduni na Maendeleo, wazo ambalo
linatarajiwa kuridhiwa na Wajumbe wa SECAM watakapokutana kwenye mkutano mkuu wa kumi
na sita, Julai, 2013, nchini DRC.
Warsha hii ambayo ilikuwa chini ya uongozi
wa Kardinali Polycarp Pengo, Rais wa SECAM, imehudhuriwa pia na Askofu mkuu Barthelemy
Adoukonou, Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni. Wengine walikuwa ni Kardinali
Theodore Adrien Sarr, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dakar, Senegal ambaye ni Makamu
wa kwanza wa Rais SECAM.
Washiriki wa Warsha hii wamechambua kuhusu majadiliano
ya kitamaduni na kiimani Barani Afrika; fursa, changamoto na matatizo Barani Afrika
katika mchakato wa maendeleo; utandawazi, usasa, utawala bora pamoja na sera za maendeleo
kwa Bara la Afrika