2012-11-23 15:06:20

Kardinali mteule James Michael Harvey ateuliwa kuwa Mhudumu Mkuu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo, Nje ya Kuta


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Kardinali mteule James Michael Harvey mwenye umri wa miaka 63 kuwa Mhudumu Mkuu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo, Nje ya Kuta. Alizaliwa tarehe 20 Oktoba 1949, nchini Marekani.

Baada ya kuhitimu masomo na majiundo yake ya kikasisi, alipadrishwa kunako tarehe 29 Juni 1975 kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Milwaukee. Kwa muda wa miaka 30 amefanya utume wake mjini Vatican kwa nafasi mbali mbali kuanzia mwaka 1982. Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili tarehe 29 Septemba 2003, kuwa Askofu mkuu na kiongozi mwandamizi wa Makao ya Papa.

Tarehe 24 Oktoba 2012 Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, akamteua kuwa Kardinali.







All the contents on this site are copyrighted ©.