Tanzania inapania kupata Katiba Mpya na nchi kuendelea kuwa na amani na umoja wa kitaifa!
Rais Jakaya Kikwete Jumatano tarehe 21 Novemba, 2012 katika Ikulu ya Dar-Es-Salaam,
amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon, zilizowasilishwa
na Bw. Serge Mickoto. Katika salamu hizo, Rais Bongo amemtaka Rais Kikwete kuendeleza
ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili katika nyanja mbalimbali.
Rais
Kikwete amemwambia mjumbe huyo wa Rais Bongo, kuwa Tanzania inathamini ushirikiano
uliopo na juhudi za kuuendeleza ushirikiano huu ni muhimu kwa nchi zote mbili.
Mapema
asubuhi Rais Kikwete amepokea hati za utambulisho za mabalozi kutoka Iran na Canada.
Wa kwanza kuwasilisha hati zake ni balozi Mehdi Agha Jafari na kufuatiwa na Balozi
wa Canada Bw. Alexandre Leveque. Mara baada ya kupokea hati zao Rais Kikwete amefanya
mazungumzo na Mabalozi hao na kuwaeleza hali ya kisiasa na ushirikiano baina ya nchi
zao na Tanzania.
Rais amemueleza Balozi wa Canada kuhusu mchakato wa Katiba
unaoendelea nchini sasa hivi na kumueleza kuwa anatarajia kuwa nchi itapata Katiba
itakayohakikisha nchi inabakia kuwa na Amani na Umoja. “Tunataka kuhakikisha kuwa
Umoja wa Kitaifa unabakia, hakuna migawanyiko ya kidini wala kikabila, tunataka Katiba
ambayo haitaleta migawanyiko ya aina yeyote wala kupendelea kundi lolote nchini Mwetu”
Rais amesisitiza.