2012-11-17 09:22:35

Maaskofu Katoliki Kenya wafanya uteuzi wa baadhi ya watendaji wake wakuu


Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya limemteua Sr. Esther Wangui Kimani kuwa Mratibu mpya wa Mashirika ya Kipapa ya Utoto Mtakatifu nchini Kenya, uteuzi ambao utaanza kutekelezwa hapo Januari 2013.

Sr. Kimani anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Sr. Jane Nugi wa Shirika la Consolata ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Mkuu wa Shirika la Waconsolata na hivyo kulazimika kuhamia nchini Tanzania.

Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya katika mkutano wake, uliohitimishwa hivi karibuni umemteua Mama Jacinta Kathamu Mutegi kutoka katika kitengo cha misaada Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya ili kuwa Katibu mtendaji, Idara ya Afya Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya, uteuzi ambao unaanza mara moja. .

Wakati huo huo, Maaskofu Katoliki Kenya, wamemteua Bwana Stephen Mwalyo Kituku aliyekuwa katibu mkuu mtendaji wa Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki nchini Kenya, Caritas kuwa Mkurugenzi wa muda wa Caritas, Kenya, kisheria.







All the contents on this site are copyrighted ©.