2012-11-13 09:57:21

Litania katika maadhimisho ya Mwaka wa Imani


Mama Kanisa anaendelea kuwahimiza watoto wake kuhakikisha kwamba, wanatolea ushuhuda amini wa imani yao kwa Kristo na Kanisa lake, katika maadhimisho ya Mwaka wa Imani. Sanaa mbali mbali zinaweza kutumika katika kufikisha maudhui ya imani kwa urahisi zaidi. Soma na fanya tafakari ya kina baada ya litania hii ambayo mwamini mmoja ameitunga wakati huu wa maadhimisho ya Mwaka wa Imani. Huu ni muhtasari wa Ukuu wa Fumbo la Utatu Mtakatifu.

Baba wa mbinguni, muumba wa ulimwengu, chanzo cha wema wote;
Kiitikio: Fungua mlango wa imani kwa ajili yetu.
Baba, Nafsi ya Kwanza, ya Utatu Mtakatifu sana;
Baba wa Mwana wa Pekee
Baba na Mwana, anapotoka Roho Mtakatifu;
Baba wa uzuri na hekima;
Baba uliye wa milele, ukuu wa shani kubwa na utakatifu;
Baba mwenye uwezo wote, upole na huruma yote;

Yesu, Mchungaji wetu wa daima, unatupatia neema yako ya uponyaji;
Kiitikio: Utuwezeshe kuishi kwa imani.
Yesu, uliyeko katika Ekaristi, utudumishe katika imani yetu;
Yesu, uliyetabiriwa na manabii, lifungue Neno lako kwetu;
Yesu, kiongozi wa mataifa yote, utuongoze kwa upendo wako;
Yesu, ndani yako, pamoja na Baba na Roho Mtakatifu, tu wamoja

Roho Mtakatifu wa upendo na ukweli, wa hekima na ufahamu;
Kiitikio: Uje na uikuze imani yetu.
Roho Mtakatifu, unayeifanya upya sura ya dunia;
Roho Mtakatifu, angaza mwanga wako katika roho zetu;
Roho Mtakatifu, chora sheria yako katika mioyo yetu;
Roho Mtakatifu, tuwashe moto wa mapendo yako;
Roho Mtakatifu, tufundishe kusali na utuongoze sisi katika njia ya wokovu;

Kwa kuabudu kwetu Sakramenti Takatifu;
Kiitikio: Ifanye imani yetu ifikie ukamilifu.
Kwa Mwili wako Mtakatifu sana na Damu yako;
Kwa zawadi ya Ekaristi;










All the contents on this site are copyrighted ©.