2012-11-10 07:57:52

Mwaka wa Imani uwawezeshe wanafunzi kuwa mashahidi amini wa Kristo na Kanisa lake


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemwandikia ujumbe wa matashi mema, Askofu msaidizi Lorenzo Leuzzi, wakati huu wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali mjini Roma, wanapofanya hija ya kichungaji mjini Assisi, Italia, siku ya Jumamosi, tarehe 10 Novemba, 2012, wakiongozwa na kauli mbiu "Alipokuwa angali mbali" inayotolewa kwenye sehemu ile ya Injili inayomzungumzia Baba Mwenye huruma na Mwana mpotevu.

Baba Mtakatifu katika ujumbe huu ambao umeandikwa kwa niaba yake na Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu mkuu wa vatican anabainisha kwamba, leo ya binadamu ndiyo leo ya Mwenyezi Mungu inayojidhihirisha kwa namna ya pekee, katika maeneo ya Mji wa Mtakatifu Francisko wa Assisi, shahidi amini wa Yesu na Injili yake.

Mwanzoni mwa Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, Baba Mtakatifu anapenda kuwatakia kila la kheri wanafunzi wanaofanya hija hii ya maisha ya kiroho kwamba, mfano na maisha ya Mtakatifu Francisko wa Assis, Msimamizi wa Italia, utaibua kwa namna ya pekee miongoni wa vijana hamu ya kuwa mashahidi waaminifu kwa Kristo na Kanisa lake, kwa kuhakikisha kwamba, Habari Njema ya Wokovu inaendelea kuleta upya wa maisha. Mwishoni, anawatakia kila la kheri na baraka tele katika Mwaka wa Masomo uliofunguliwa hivi karibuni.







All the contents on this site are copyrighted ©.