Monsinyo Angelo Vincenzo Zani ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Elimu
Katoliki
Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Monsinyo Angelo Vincenzo Zani kuwa
Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki na kumpandisha hadhi ya kuwa ni
Askofu mkuu. Kabla ya uteuzi wake, alikuwa ni Katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa
la Elimu Katoliki.