Ujumbe wa Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican kwa wasomi
Baba Mtakatifu Benedikto XVI, katika viwanja vya Mt Petro Mjini Vatican, mnamo tarehe
11Oktoba 2012 anapofungua Mwaka wa Imani utakaofungwa katika Sherehe ya Yesu Kristo
Mfalme 2013 ametupatia ujumbe sisi wasomi na watafiti akirudia maneno ya Baba Mtakatifu
Paulo VI. Anasema, wapendwa
enyi watu watafuta ukweli, watu wa kufikiri na wanasayansi, watafiti juu ya mwanadamu,
dunia, historia na wote walio mahujaji katika kuuendea mwanga wa UKWELI. Mama Kanisa
daima yupo kwa ajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na hivi kutafuta ukweli, kuishi
ukweli na kulinda ukweli huo. Ndiyo kusema kuwa makini, akizama katika ujumbe wa ukweli
ambao amekabidhiwa toka kwa Kristo. Katika hilo Mama Kanisa huweka nguvu iliyojaa
unyenyekevu kwa Roho wa ukweli. Wapendwa wasomi na watafiti baada ya utangulizi
huu, Baba Mtakatifu anatuambia sisi wasomi na watafiti akisema, njia yenu ni yetu,
wala njia yenu si ngeni kwetu. Mama Kanisa ni rafiki wa wote na rafiki wa wito wenu
kama watafiti na wasomi. Mama Kanisa yuko pamoja nanyi katika mahangaiko na matamanio
yenu ya mafanikio, na wakati inapofaa na kuhitajika Mama Kanisa huwafariji katika
kutofaulu kwenu na pale mnapokatishwa tamaa. Kwenu ninyi wasomi na watafiti bado
tunao ujumbe na ujumbe ndo huu: Endeleeni kutafiti bila kuchoka na bila kupindisha
ukweli. Kumbukeni maneno ya mmoja wa marafiki zenu wakuu, Mt. Augustino anayesema,
njooni tutafute, tukiwa na hamu ya kutafuta, na tutafute tukiwa na hamu ya kugundua
zaidi. Toka hamu ya kutafuta na kugundua ukweli katika upole na unyenyekevu kuna
heri za Mungu. Si hilo tu bali, kwa wale wote ambao pamoja na kuwa na ukweli na kuutunza
wanazidi kuwa wanyenyekevu kutafuta mbinu za kuufanya uwe wazi zaidi na kuweza kufikisha
na kuushirikisha kwa wengine. Mama Kanisa aona heri kwa wale wote ambao hawajaona
ukweli lakini wanazidi kuutafuta kwa moyo mkunjufu. Kwa jinsi hiyo Mama Kanisa anasema
ingekuwa vema kutafuta mwanga wa kesho kwa kutumia mwanaga wa leo hadi kufikia ukamilifu
wa mwanga wenyewe. Baba Mtakatifu anatukumbusha sisi wasomi na wanasayansi juu
ya kufikiri, yakuwa KUFIKIRI ni jambo nyeti, kwa hakika ni kazi, kwa maana hiyo ole
wao wanaofunga macho yao makusudi, ili wasione ukweli! KUFIKIRI ni wajibu na hivi
kama mmoja anatengeneza roho ya gizagiza kwa mbinu lukuku, akiifisha na kuifanya na
kuifanya iwe na kiburi basi azama katika hatari kubwa! Kumbe yafaa daima kujiuliza
ni Je, ni mwongozo upi ulio wa uhakika kwa wanasayansi na wasomi kwa ujumla zaidi
ya kufikiri vizuri katika njia ya mwanga? Wapendwa wasomi na wanasayansi, bila
kupoteza muda Mama Kanisa anakuja kwetu kutupatia njia angavu ya mwanga fumbo, ambayo
ni IMANI. Mwanga fumbo watoka kwake yeye aliye MKOMBOZI wa ulimwengu, Kristu mfufuka,
anayesema daima “Mimi ni nuru ya ulimwengu, mimi ni njia, ukweli na uzima” Baba
Mtakatifu anaendelea kusema, maneno haya yakumbukeni, Sayansi yautumikia ukweli na
imani yautumikia ukweli. Kuweni na uhakika katika imani rafiki mkuu wa akili na mang’amuzi.
Jiendeleze katika kuupata mwanga wa imani ili uweze kuukamata ukweli, ukweli wote. Mama
Kanisa awatakia matumaini na mafanikio katika shughuli nyeti hiyo ya kutafuta na kusimamia
ukweli ambao utakupatia uhuru na heri na Baraka za Mungu. Amina Ujumbe huu wafikishwa
kwako na Pd. Richard Tiganya, C.PP.S.