2012-11-08 09:27:01

Benedikto XVI kutembelea wazee kama sehemu ya maadhimisho ya Mwaka wa Wazee na mshikamano kati ya kizazi na kizazi


Katika maadhimisho ya Mwaka wa Wazee Barani Ulaya na Mshikamano kati ya kizazi na kizazi, uliotangazwa na Umoja wa Ulaya, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Jumatatu tarehe 12 Novemba 2012, anatarajiwa kutembelea nyumba ya wazee wanaohudumiwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, hapa Roma, kama kielelezo cha mshikamano wa Kanisa na Wazee.

Baada ya kupokelewa na wenyeji wake, Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, atawatembelea wanandoa wawili wazee ambao walinusurika kifo wakati wa tetemeko la ardhi lilipoikumba Haiti, Mwezi Januari, 2010. Atawatembelea wazee wengine kwenye vyumba sita na baadaye, atakutana na Jumuiya ya Wazeee, watu wanaojitolea pamoja na wanachama wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio.

Baba Mtakatifu atapata fursa pia ya kusalimiana na vijana watakaokuwa wamekusanyika nje ya Makazi ya wazee wanaohudumiwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, yenye makao yake makuu hapa mjini Roma.







All the contents on this site are copyrighted ©.