2012-11-07 14:55:03

Rais Baraka Obama aibuka kidedea katika kinyang'anyiro cha Urais Marekani


Baada ya patashika nguo kuchanika, katika kinyang’anyiro cha kuwania kwenda Ikulu Marekani, Rais Baraka Obama amembwaga mpinzani wake Mitt Romney na hivyo kufanikiwa kuingia Ikulu kwa mara ya pili.
Rais Obama amemshukuru pia mpinzani wake kwa changamoto kubwa alizozionesha hadi dakika ya mwisho ya kampeni za uchaguzi ambazo zimegharimu takribani dolla billioni moja za kimarekani. Amewashukuru wapiga kura wake ambao wamemwezesha tena kurudi Ikulu kwa kipindi kingine cha miaka minne. Masuala ya uchumi na maendeleo ya wananchi wa Marekani ni kati ya mambo yaliyopewa kipaumbele cha kwanza wakati wa kampeni ya vuta nikuvute nchini Marekani.








All the contents on this site are copyrighted ©.