Uchumi wa Tanzania unacharuka, lakini wakulima vijijini wamesahaulika!
Taarifa ya Benki ya Dunia inaonesha kwamba, uchumi wa Tanzania unaendelea kukua na
kuboreka siku hadi siku, lakini kwa bahati mbaya, wakulima vijijini wamesahaulika
katika mchakato huu, ingawa kilimo kimekuwa ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania.
Benki
ya Dunia inabainisha kwamba, uchumi wa Tanzania katika kipindi cha mwaka 2013 na 2014
unatarajiwa kukua kwa asilimia 6.5 hadi 7. Sekta zinazoongoza kwa sasa ni madini,
taasisi za fedha na mawasiliano. Matumaini ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni kutokana
na kugunduliwa kwa gesi asilia na mafuta nchini Tanzania. Uzalishaji wa nishati hii
unaweza kuanza katika kipindi cha miaka saba hadi kumi kuanzia sasa.
Sera ya
Kilimo Kwanza, inayopewa msukumo wa pekee na Serikali ya Tanzania, inaweza kuleta
mabadiliko katika maisha ya wakulima wengi vijijini, ili kuendelea kuchangia katika
ukuaji wa uchumi wa Tanzania.