2012-11-03 13:27:16

Monsinyo Guido Pozzo ateuliwa kuwa mkuu wa kitengo cha sadaka ya Papa


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amekubali kung'atuka kutoka madarakani kwa Monsinyo Fèlix del Blanco Prieto aliyekuwa mkuu wa kitengo cha sadaka kutokana na kutimiza umri wa kustaafu na badala yake, Baba Mtakatifu amemteua Monsinyo Guido Pozzo, ambaye hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Katibu mkuu wa Tume ya Kipapa ya Kanisa la Mungu "Ecclesia Dei" na kumpandisha hadhi ya kuwa Askofu mkuu.

Askofu mkuu mteule Guido Pozzo alizaliwa Italia kunako tarehe 26 Desemba 1951. Akapadrishwa tarehe 24 Septemba 1977. Alianza kutoa huduma za kitume kwenye Baraza la Kipapa la Mafundisho Sadikifu ya Kanisa tarehe 4 Mei 1987. Tarehe 18 Julai 2009 akateuliwa kuwa Katibu mkuu wa Tume ya Kipapa ya Kanisa la Mungu







All the contents on this site are copyrighted ©.