Papa kuwakumbuka na kuwaombea Marehemu Makardinali na Maaskofu waliofariki dunia kutoka
sehemu mbali mbali za dunia: 2011 - 2012.
Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Jumamosi tarehe 3 Novemba 2012, anatarajiwa
kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu, kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea Marehemu
Makardinali, Maaskofu wakuu na Maaskofu waliofariki dunia katika kipindi cha Mwaka
2011 hadi Oktoba 2012.
Takwimu zinaonesha kwamba, katika kipindi cha Mwaka
uliopita, kuna jumla ya Makardinali 10 waliofariki dunia. Kuna Jumla ya Maaskofu 143,
ambao pia wametangulia mbele ya haki wakiwa na tumaini la ufufuko wa wafu na maisha
ya uzima wa milele. Kati ya Maaskofu hao, kuna jumla ya Maaskofu 21 kutoka Afrika.
Maaskofu
wafuatao ni wale waliofariki dunia kutoka katika Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu
Katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA:
1. Askofu Augustini Misago wa Jimbo
Katoliki Gikongoro, Rwanda: 12 Machi 2012. 2. Askofu mstaafu Joseph Nduhirubusa
wa Jimbo la Ruyigi, Burundi: 16 Julai 2012. 3. Askofu Pascal W. Kikoti wa Jimbo
Katoliki Mpanda, Tanzania: 28 Agosti 2012. 4. Askofu mstaafu Patrick A. Kalilombe,
Jimbo Katoliki Lilongwe, Malawi: 25/9/ 2012 5. Askofu mstaafu Joseph B. Williger,
Jimbo Katoliki Jinja, Uganda, 30/9/ 2012. 6. Askofu mstaafu Felix E. Mkhori, Jimbo
Katoliki Lilongwe, Malawi, 17/10/ 2012.