Licha ya vipingamizi na changamoto nyingi zinazo onekana duniani dhidi ya imani,
Mungu bado anaipenda dunia.
Padre Federico Lombardi, ameeleza katika tahariri
yake ya wiki hii, akitazama kwa makini, tafakari za Kanisa, juu ya haja ya uinjilishaji
mpya, katika dunia ya leo, ambamo mnaonekana watu wengi , kuwa na mwelekeo wa kutaka
kujitenga na imani kwa Mungu. Pia mnamo onekana kuwa na vipingamizi na changamoto
nyingi zinazo pambana na utangazaji wa Injili, katika maeneo mbalimbali duniani,
katika nyakati hizi .
Padre Fedrico Lombardi amerejea Ujumbe wa Sinodi ya
Maaskofu uliotolewa kabla ya sinodi hiyo kufungwa, unaolitaka kanisa kutokatatamaa
bali, lijitokeza kwa ushupavu kuhubiri Injili ya upendo wa Mungu kwa watu, likiwa
limesimama imara katika imani yake kwa Mungu, kwa nguvu za ushuhuda hai wa Kristo
Mfufuka na Roho wake.
Na kwamba, hakuna sababu za kuyaona yote kuwa batili
katika utandawazi,malimwengu na matukio mapya ya jamii, likiwemo wimbi la uhamiaji.
Badala yake vyote hivyo vinapaswa kuchukuliwa na Kanisa kama fursa za uinjilishaji.
Na
vipengere vingi vilivyowasilishwa katika majadiliano ya Sinodi ya Maaskofu waliokusanyika
kutoka pande mbalimbali za dunia, juu ya ufanyaji upya Kanisa katika maisha ya familia,
parokia, Makleri na walei, ni kutokana na utambuzi kwamba, ni utume wa Kanisa kwa
familia ya binadamu.
Kanisa daima katika majadiliano juu ya ulimwengu na matatizo
yake, katika mitazamo ya tamaduni, sayansi, elimu, sanaa, huduma , pia katika nyanja
za uchumi, ajira na siasa, hufanyika kama sehemu ya huduma ya kufanikisha mema
kwa wote.
Na kwa namna pekee, ni Kanisa hulenga kujenga ushirikiano na waumini
wa dini nyingine, na katika ukweli kwamba, Kanisa haliwezi kujitenga lenyewe, kama
kisiwa, bali linapaswa kuuishi imani yake kwa uaminifu ndani ya jamii, mchanganyiko,
likiendelea na kazi yake ya kutolea sala na sadaka, na kutambua uwepo wa Mungu kupitia
watu wahitaji maskini na fukara wa kiroho.
Padre Federico Lombardi amemalizia
tahariri yake kwa kutazama utume wa Maaskofu, katika mazingira yao halisi, kwamba
kwa sasa wanaagana na Papa - ambaye kwa uaminifu ameandamana nao katika kazi nzito
ya Sinodi , ambamo pia alitoa mchango wake wa kina. Na kwamba, wanatawanyika wakiwa
wametiwa nguvu na Mwaka huu wa imani, wakijisikia kuhamasika zaidi katika kutafuta
njia , fursa na namna za kuwashirikisha wote, kutangaza uzuri wa imani, yenye thamani
zaidi ya vitu vyote vilivyopo.