2012-10-27 15:13:28

Papa ateua wajumbe wapya katika Mabaraza mbali mbali ya Kipapa


Baba Mtakatifu ameteua wajumbe wa Baraza la Kipapa linaloratibu misaada ya Kanisa Katoliki Duniani "Cor Unum", nao ni:
Kardinali Oscar Andrés RODRÍGUEZ MARADIAGA, S.D.B., Askofu Mkuu wa Tegucigalpa (Honduras) na Rais wa Caritas Internationalis. Wengine ni:
Askofu Mkuuu Alberto TAVEIRA CORRÊA, wa Jimbo Kuu la Belém do Pará (Brasile); Askofu Mkuu Paolo PEZZI, F.S.C.B., wa Jimbo Kuu la Mama wa Mungu Moscow, Askofu Tarcisius Isao KIKUCHI, S.V.D., wa Jimbo la Niigata (Japan),na Makamu wa Rais wa Caritas Internationalis kwa ajili ya Asia; na pia ni mwakakilishi katika mashirika.

Wengine ni Mons. Peter NEHER, Rais wa Deutscher Caritasverband – Ujeruman, Mons; Francesco Antonio SODDU, Mkurugenzi wa Kitaifa wa Caritas Italiana; Mheshmiwa Barone Johannes Nepomuk HEEREMAN VON ZUYDTWYCK, Rais Mtendaji wa Shirika la Msaada katika Kanisa Hitaji;
Dr. Carolyn Y. WOO, Rais wa Shirika la Misaada Katoliki Marekani - U.S.C.C.na Bi Maritza SÁNCHEZ ABIYUD, Mkrugenzi wa Caritas Cuba.
Aidha Papa amemteua Dott. Michel ROY, Katibu Mkuu wa Caritas Internationalis kuwa mshauri wa Baraza hili la Kipapa.

Baba Mtakatifu pia ameteua wajumbe wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Majadiliano na dini zingine kama ifuatavyo:
KardinalI Fernando FILONI, Mkuu wa shirika kwa ajili ya Uinjilishaji wa watu,
Askofu Mkuu Peter Takeo OKADA, wa Jimbo Kuu la Takei Tokyo (Japan;
Askofu Mkuu Jean Benjamin SLEIMAN, O.C.D., wa Jimbo Kuu la Baghdad ya Mashariki (Iraq);
Askofu Mkuu Daniel Joseph BOHAN,wa Jimbo Kuu la Malkia (Canada);
Askofu Mkuu Salvatore FISICHELLA, Askofu Mkuu wa Jina wa Voghenza, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji Mpya ;
Askofu Michel DUBOST, C.I.M., wa Jimbo la Evry-Corbeil-Essonnes (UFransa); Askofu Angelito R. LAMPON, O.M.I., Askofu wa Jina wa Valliposita, Vika wa Jimbo la Kichungaji la Jolo (UFilippine);
Askofu Francesco BIASIN, wa Jimbo la Barra do Piraí-Volta Redonda (Brazil); Askofu Joseph Chusak SIRISUT, Jimbo la Nakhon Ratchasima (Thailand);
Askofu Sebastian Francis SHAH, O.F.M., Askofu wa Jina wa Tino,
Pamoja na Askofu Msaidizi wa Lahore (Pakistan); Askofu Michael Didi Adgum MANGORIA, Askofu mwandamizi wa Jimbo la El Obeid (Sudan);
Askofu e Tomo VUKŠI, wa Jimbo la Kijeshi la Bosnia ed Erzegovina; Askofu Matthew Hassan KUKAH, wa Jimbo la Sokoto (Nigeria).

Wakati huohuo, Jumamosi Papa alikubali ombi la kujiuzuru kazi za Kichungaji za Jimbo la Pemba, Msumbiji, lililotolewa na Askofu Ernest Maguengue , kwa mujibu wa sheria za Kanisa namba 401 kipengere namba 2.
Katika nafasi yake Papa amemteua Padre Fernando Domingos Costa CP, kuwa msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki Pemba, Msumbiji.








All the contents on this site are copyrighted ©.