2012-10-26 15:51:19

Ujumbe wa Mababa wa Sinodi kwa ajili ya Watu wa Mungu


Maadhimisho ya Sinodi ya kumi na tatu ya Kawaida ya Maaskofu, iliyoongozwa na kaulimbiu:” Uinjilishaji Mpya: Utangazaji wa Imani ya Kikristo”, Ijumaa hii, 26 Oktoba 2012, katika kikao chake cha ishirini, majira ya asubuhi, Mababa wa Sinodi walikusanyika kwa ajili ya kusoma na kupitisha ujumbe wa mwisho ya Sinodi, kwa ajili ya Taifa la Mungu yatakayopelekwa kwa Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ili aweze kuyafanyia kazi wakati akitayarisha Waraka wake wa kitume mara baada ya Maadhimisho ya Sinodi.

Ujumbe umetolewa katika vifungu kumi na nne kama ifuatavyo.

1. Kama maji ya uzima Jangwani.
Kama ilivyokuwa kwa mwanamke Msamaria katika kisima cha Yakobo ( Yohane 4, 5-42), vivyo hivyo Kanisa lina kiu na linapaswa kuketi karibu na watu, wake kwa waume wa wakati huu , likiionyesha uhai wa Bwana, mwenye kuwa na maji ya uzima wa milele katika maisha yake , ili watu waweze kusadiki na kukutana Nae.

2. Uinjilishaji Mpya – Uweze kuwaongoza wake kwa waume wa nyakati zetu kwa Kristo kukutana naye katika kila kona , kama hoja ya kidharura kwa watu wote duniani , iwe katika mataifa makongwe au mapya katika uinjilishaji.

3. Kukutana binafsi na Kristo ndani ya Kanisa, muumini anaalikwa kuitafakari sura ya Kristu na kuzama ndani ya fumbo la wokovu, na kuishi kwa majitolea ya kweli hadi kifo cha Msalaba, na kuipokea zawadi ya Baba ya ufufuko wa kutoka kwa wafu, na msaada wa Roho Mtakatifu aliyedhaminishwa kwetu .

4.Kukutana na Kristo: kusikiliza na kusoma Maandiko , kwa kuyaishi maisha ya Mitume wa Yesu, Petro, Andrea, Yakobo na Yohane. Na pia kuwa na hamu ya kumwona Yesu kama iliyo kuwa kwa Zakayo, au kwa mtu kipofu, au a kwa Martha na Maria... kusoma Maandiko Matakatifu mara kwa mara kwa mwanga wa maongozi na Mafundisho sahihi ya Kanisa.

5.Kujiinjilisha binafsi na kuongoka,Mababa wa Sinodi wanasema, Ole wao wale wale wanaofikiria Uinjilishaji mpya, si kwa ajili yao wenyewe. Kipengere hiki kinatoa wito wa kuiishi Injili ya Kristo , kwa ajili ya wongofu binafsi.

6. Kukumbatia kila mwanya katika dunia ya leo kama nafasi ya uinjilishaji, na bila ya kusijikia kutishwa na hali tuziishizo kwa wakati huu, kama ilivyo kwamba leo hii dinia imejaa hali za vitisho na changamoto. Lakini upendo wa Mungu kwa viumbe wake, haupungui, na hivyo kanisa linapaswa kuendelea kueneza Neno lake kwa kurejesha matunda mapya.

7. Uinjilishaji ndani ya familia na maisha yaliyowekwa Wakfu
Tangu mwanzo wa utangazaji wa habari Njema ya Wokovu, uenezaji wa Imani umepata makazi yake, kizazi hadi kizazi, ndani ya familia ambamo kwa namna ya pekee, wajibu wa wake kwa waume, unakuwa ni mhimili wa imani kwa kizazi chipukizi. Wazazi wakiwa walimu wa kwanza wa ukweli na majiundo ya maisha yaliyozamishwa katika sala, shuhuda za matunda ya upendo unaoonekana kwa watoto na vijana kupitia huduma za kifamilia.

8. kwa Jumuiya ya Kanisa na kazi za kitume
Mababa wa Sinodi wanasema, kazi za Uinjlishaji, kikanisa hazina mwenyewe, bali ni za Jumiya nzima ya kanisa kwenye mitazamo mbalimbali. Jumuiya kama chombo cha kufanikisha mtu kukutana na Yesu, iwe kupitia usomaji wa Maandiko Matakatifu, maisha ya Kisakramenti, mshikamano wa kijamii, matendo ya huruma, na utume.

9. Ili vijana waweze kukutana na Kristo
Katika juhudi hizi za Uinjilishaji mpya, Vijana ni mtima, na sababu kuu ni kwa kuwa wao ni sehemu muhimu wa uwepo ubinadamu na kanisa, hata katika mustakhabali wake.

10. Ili Injili izame katika majadiliano na tamaduni na uzoefu wa ubinadamu na dini zingine.
Uinjilishaji Mpya kiini chake ni Kristo, mwenye kuw ana hali zote za ubinadamu, kuuona uwezekano halisi wa kukutana nae Kristu. Hii ina maana kwamba, kuwa na huduma maalum, kupitia majadiliano na mshikamano katika uwaminifu wa kila mmoja , kuipanda “mbegu ya Neno". Hasa, Uinjilishaji Mpya unahitaji muungano mpya kati ya imani na hoja, katika kishawishi cha imani .

11.Katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani , miaka 50 ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican na rejea katika Katekisimu Mpya ya Kanisa Katoliki,
Maababa wa Sinodi pia wametoa umuhimu wa kuyatazama matukio haya kwa makini kwa ajili ya kusaidia mchakato unaopania kuleta wongofu wa ndani na utakatifu wa maisha.

12. ili kutafakari kwa kina fumbo la maisha na mahangaiko yake
Mababa wa Sinodi wameonyesha kujali si tu masuala ya kiroho lakini pia mahitaji ya kimwili kwa kuyatazama mahangaiko ya watu katika maisha hasa kwa maskini na wanao teswa wa hali zingine mbalimbali kama maradhi, vita na dhuluma. Yote hayo yanahitaji huduma ya upendo wa kina wenye kujitolea mhanga kwa aji

13, Neno kwa Makanisa katika maeneo mbalimbali ya duniani.
Mababa wakiwa wameugana katika umoja wao kwa namna ya pekee wametoa wito kwa waamini wa Kristu, kujenga umoja , kama silaha ya kumshuhudia Kristo , katika juhudi hizi za Uinjilishaji Mpya.


14.Bikira Maria, Mwanga wa Uinjilishaji Jangwani,

Mababa wa Sinodi wamehitimisha Ujumbe wao kwa kutoa msisitizo wa kushirikiana na Khalifa wa Mtakatifu Petro, kama Yesu alivyo waambia Mitume wake, “Nendeni , mkawafanye watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi wangu ...”
Pia wameyataja maneno ya Maria , kuwa mhimili wa njia hii ya Unjilishaji Mpya , hasa katika kujifunua kwa ukame wa maisha ya kiroho, na Jangwa la ndani . Ni msaada wa kutambua hitaji msingi la kutembea na Yesu katika ukweli wa Neno lake, Mkate unaolisha udugu wa Jumuiya za Kikanisa na upendo wa kweli. Maji ya uzima yanayotililika kutoka Jangwani .








All the contents on this site are copyrighted ©.