Mapema Alhamis, Papa alimpokea Rais Demetris Christofias, Rais wa Jamhuri ya Cyprus.
Na baadaye Rais huyo alikutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Tarcisio Bertone, akiwa
na Katibu wa Mahusiano na Nchi zingine, Askofu Mkuu Domenique Mamberti. Maongezi
ya viongozi hawa yalifanyika katika hali ya urafiki na mazunguzo , yakielnga zaidi
katika uimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Jimbo la Papa na Jamhuri ya Cyprus.
Pia waliweze kuzungumzia mambo yanayogusa nchi zote mbili , na hasa umuhimu wa majadiliano
kati ya jamii, na haki za binadamu kuheshimiwa, ikiwemo uhuru wa kidini. Kwa
kuwa Jamhuri ya Cyprus kwa wakati huu ni Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, pia walitazamisha
mawazo yao katika hali za bara la Ulaya kwa wakati huu. Na walionyesha tumaini lao
kwamba, , juhudi zinazofanyika kupitia njia za majadiliano,kati ya pande zinazo pingana
Mashariki ya kati , hatimaye zitaweza kufanikisha mchango unaofaa kwa jumuiya ya kimataifa
kudumisha amani katika eneo hili.