Idhaa ya Kiswahili ya Redio Vatican, inawatangazia wasikilizaji wa Afrika Mashariki
na Kati kwamba, tangu Jumapili 28 Oktoba 2012, Matangazo yatasikika kila siku katika
masafa mafupi "shortwave" ifuatavyo, mitabend 41 kHz 9960 , na mitabendi 25 kHz
11625. Muda unabaki uleule, saa moja za jioni na vipindi kurudiwa mapema asubuhi,
saa kumi na mbili na nusu kwa saa za Afrika Mashariki. Kwa wakazi wa Jiji la
Roma , kipindi kitaendelea kusikika katika masafa ya FM 103.8. Lakini muda unabadilika
, itakuwa majira ya saa kumi na moja za jioni badala ya saa kumi na mbili za Jioni
na kurudiwa mapema asubuhi saa kumi na nusu za asubuhi. Tunaomba radhi kwa usumbufu
utakaojitokea.