Muhtasari wa yaliyojadiliwa katika Sinodi wiki hii
Jumapili hii, inapita wiki moja, tangu Baba Mtakaifu Benedikto XVI, alipozindua Sinodi
13 ya kawaida ya Maaskofu, inayoongozwa na Madambiu: Uinjilishaji Mpya, Uenezaji
wa Imani ya Kikristu.
Kwa muhtasari, Mababa wa Sinodi wiki hii, wameweza kusikiliza
maelezo , maoni, shuhuda na na uzoefu, juu ya hoja zinazogusa moyo wa kanisa, kama
ulegevu wa imani, madhulumu dhidi ya Wakristu na watu maskini, madhulumu ya ngono
kwa makundi manyonge, kama watoto na wanawake. Kipeo cha miito ya Upadre na maisha
Matakatifu, mahusiano kati ya Sayansi na Imani, umuhimu wa elimu katika jamii, utandawazi
na madhara yake na umuhimu wa vyombo vya habari katika katika huduma ya uinjilishaji
mpya.
Isabella Piro wa Redio Vatican , akitoa muhtasari huo, ameelelza kwamba,
Mababa wa Sinodi , kwa ujumla wamezungumzia nshikamano na umoja wa dini, unaolenga
kutobadili nia za dini na kuzuia dini kugeuzwa kuwa uwanja wa Kisiasa. Wasisitiza
dini ibaki kuwa chombo cha amani, ni wazo lililotawala majadiliano ya Sinodi siku
ya Ijumaa.
Pia sinodi imetazama kashfa za madhulumu ya ngono hasa yanayofanywa
na watumishi wa Kanisa wabovu. Maaskofu wamesema kanisa lisiogope kupata habari hizo,
na uinjilishaj mpya ni lazima uwakumbatie kafara kwa kuwasikiliza na moyo wa upendo
na unyenyekevu, na kutafuta mbinu za kuponya uchungu wa fikira na kurudisha imani
yao. Na kwa ajili ya kuzuia na hasa madhulumu kwa watoto , Maaskofu wameshauriana
kwamba ni muhimu kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya watoto na makundi dhaifu.
Na ili hilo lifanikishwe ni muhimu Kanisa, lifanye mabadiliko katika mifumo yake
ya huduma.
Aidha Mababa wa Sinodi wameshirikishana mawazo na uzoefu juu ya
kipeo cha imani na kipeo katika maisha ya Kipadre, na hasa wakitazama yanayosababisha
uhaba wa miito katika Upadre na maisha yaliyotiwa wakfu, hasa kwa nchi za Magharibi.
Hisia za Maaskofu wengi zilielemea katiak kuona kwamba, pengine inatokana na upungufu
wa uaminifu kwa wale ambao wameahidi kuushi Ukristu wao kwa kulitumikia kanisa kama
Padre au mtawa. Wamesema, kama mhubiri mwenyewe anaonekana kuwa na masiha tofauti
na kile anachokihubiri au anachotazamiwa kukishuhudia kimaisha , ni wazi watu hupoteza
onjo la kuingia katika maisha hayo.
Pia walisisitiza umuhimu wa kuchagua wenye
kuwa na wito wa kweli katika kumtumikia Mungu na Kanisa lake na si zilizofichika zinazolenga
kukimbia mambo mengine yanayomzonga mtarajiwa. Wamesema, iwapo ujumbe wa Injili si
msingi a imani ya mtu, au si lengo la Padre mwenyewe, basi maisha ya padre huyo ni
lazima yatakuwa na kasoro kikanisa.
Hoja ingine iliyotolewa maoni ni suala
la umaskini, si umasikini wa mtu lakini pia umasikini wa kiroho , na watu wanaobaguliwa
na jamii kutokana na hali yao , kama wagonjwa, wakimbizi, wahamiaji, na wale wanaoitwa
walaaniwa. Michango ya Maaskofu katika hili imesema, huu ni wakati kwa Ukristu kutoa
jibu linalofaa, lenye kuwakumbatia wote na hasa wanaoishi katika mataifa maskini yanayotafuta
kusonga mbele kimaendeleo. Wamesisistiza pia kanisa liwe mstari wa mbele , kusaidia
wakimbizi na wahamiaji wanaopambana na kipeo cha kubaguliwa katika hali yoyote ile.
Hapo Kanisa ndipo linatakiwa kuiishi Injili ya Msamaria Mwema, katika juhudi hizi
za Uinjlishaji mpya.
Bado sinodi ilitazama hoja ya mahusiano kati ya Sayansi
na Imani na kuona kwamba, katika ukweli wake mambo hayo hayapingani lakini huinuana,
katika kufanikisha ubinadamu zaidi. Lakini wakaonya kwa mara nyingi, kumekuwa na upotoshwaji
na kutojali na hivyo kusababisha utengano wa mawazo kati sayannsi nai mani, na kuvionesha
kama ni mambo yanayopingana daima, na kumbe kwa kutumiwa vyema ni mambo yanayoinuana.
Kwa mtazamo huo, Baraza limeshauri , Mabaraza ya Maaskofu ni muhimu kupambana na
hoja za kidharura , kupitia njia ya elimu.
Lakini pia wametahadharisha juu
ya shule na vyuo vikuu , zaidi sana Katoliki , kuwekwa chini ya udhibiti wa serikali,
na hivyo utendaji wake kushinikizwa na matakwa ya serikali, hata kama hayaendani na
imani Katoliki. Na hili limekuwa chanzo kikubwa cha upotoshwaji wa imani ya Mkristu.
Na hivyo kunaibuka haja ya kidharura, kwa Kanisa, kujenga majadiliano kati ya imani
na tamaduni , majadiliano katika lengo la kuboresha majiundo na shughuli za familia
na wahusika wengine katika uwanja wa elimu kama walimu.
Katika mazingira
hayo ya utandawazi, Ukumbi wa Sinodi ulionyesha kutambua umuhimu wa mkutano wa watu
wa kimataifa ulioanzishwa na Papa, unaofanikishwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya
utamaduni , lenye kukuza majadiliano kati ya dini na tamaduni , na watu wasioamini
Mungu lakini kindani humtafuta Mungu. Na pia n i muhimu kuwa na majadiliano kati ya
dini na hasa mahali ambako wakristu hawawezi kuishuhudia iamani yao , kutokana na
hofu za kushambuliwa na waamini wa dini inayowazunguka kama ilivyo katika mataifa
kadhaa yenye kuwa na Waislamu wengi.
Sinodi hii inahudhuriwa na Maaskofu kutoka
pande zote za dunia , Ulaya 103, Amerika 63, Afrika 50, Asia 39 na Oceania 7, wakiwepo
pia wageni maalum waalikwa na watalaam katika nyanja mbalimbali. Sinodi inakamilika
tarehe 28 Oktoba 2012